Saturday, March 26, 2016

SAKATA LA RAIA WA KIGENI KUKAMATWA NA TUMBILI HAI 61 VYOMBO VYA ULINZI VYAANZA KAZI



Serikali imeunda kikosi kazi kinachohusisha taasisi nyeti nchini kuchunguza sakata la kukamatwa kwa raia wawili wa Uholanzi wakiwa katika harakati za kusafirisha tumbili 61 kwenda nchini Albania.

Kikosi hicho kinaundwa na maofisa kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Kikosi cha Kupambana na Ujangili.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa aliwathibitishia wanahabari jana kuundwa kwa kikosi kazi hicho na kwamba, upelelezi wa sakata hilo umepamba moto.

“Upelelezi ndiyo kwanza bado mbichi, kwa hiyo siwezi kusema lolote kama lini watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa sababu upelelezi uko chini ya kikosi kazi hicho,” alisema Mutafungwa.

Juzi saa tano asubuhi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alitembelea Kituo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) kushuhudia wanyama hao.

Profesa Maghembe alisema kama kila kitu kitakwenda vizuri katika upelelezi, watuhumiwa wa kosa hilo watafikishwa mahakamani siku ya Jumanne.

Wanyama hao walikamatwa usiku wa kuamkia juzi katika uwanja huo wakati raia hao, Artem Alik Vardanyian (52) na Eduard Alik Vardanyian (44) wakiwa katika harakati za kuwasafirisha kwa kutumia ndege kubwa ya mizigo.

Hata hivyo, raia hao wa Uholanzi walikuwa na vibali vilivyotolewa na Mkurugenzi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Charles Mulokozi ambaye tayari amesimamishwa kazi kwa kashfa hiyo.

PATA MAARIFA KWA KUSOMA VICHWA VYA MAGAZETI HAPA.




























Friday, March 11, 2016

GARI LATEKETEA KWA MOTO KATIKA KITUO CHA MAFUTA HUKO SUMBA WANGA





MKUU WA WILAYA YA KARAGWE DEODATUS KINAWIRO AMALIZA MGOGORO WA ARDHI RUGERA.


Mkuuu wilaya ya Karagwe Deodatus Kinawiro ametatua mgogoro wa ardhi wa wanakijiji  cha Omkakajinja  na wamiliki wa block no5 na 6  kwa kueleza kuwa block hizo ziko ndani ya kijiji hicho na sio nje kama ilivyokuwa inafahamika hapo awali.

Akiongea na wananchi wa kijiji cha Omkakajinja Kinawiro amesema kuwa block namba 05 na 6 ambazo zilikuwa zinaleta mgogoro kwa wananchi wa kijiji hicho wakidai kuwa block hizo ziko nje ya kijiji ameeleza kuwa madai hayo sio sahihi na badala yake watambue kuwa block hizo ziko ndani ya kijiji cha Omkakajinja na mmiliki wa block anabaki kuwa mwekezaji tu.

Ameeleza kuwa block zimewekwa kwa mjibu wa sheria hivyo zinatakiwa kutumika kwa ajili ya kufugia na sio kufanyia shughili nyingine.

Wakati mkuuu wa wilaya akitoa maelezo hayo wananchi wameeleza kutoridhika wakitaka ardhi irudi mikononi mwao na sio kubaki katika mikono wa wamiliki wa ardhi kwani tangu wafukuzwe katika ardhi hiyo mwaka 1970 wanaishi kwa kutanga tanga na hawana sehemu ya kulima au kufanya shughuli nyingine za maendeleo.

Hata hivyo mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Omkakajinja amesema kuwa wako tayari kufikisha suala hili mahakamani ili kupata haki ya kumili ardhi yao huku akieeleza kutiokubaliana na maamuzi ya mkuu wa wilaya