Wednesday, October 31, 2012

WATU SABA WAFARIKI KWA KULIPUKIWA NA BOMU




Na 
    Juhudi  Felix
     Karagwe

Watu saba wakazi kijiji cha Rugarama  kata ya Ihanda wilaya karagwe wamefariki dunia baada ya kulipukiwa na kitu kilichosadikiwa kuwa ni bomu.

Tukio hilo limetokea October 30 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi katika eneo la kijiji hicho.
Jeshi la polisi wilayani humo limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo limewataja marehemu hao kuwa ni Eladius Robert(15),Fenius Frank(miaka 3 na miezi 6),Faraja Frank(mwaka 1 na mwezi 3)na wengine waliopoteza maisha kuwa ni Scatus Kamali(15),Nelson Lphonce(14)Edger Gidion(14) na mmoja ambaya jina lake ambayae halikufahamkika mara moja(17).

Inadaiwa kuwa marehemu walikuwa wanaokota vyuma chakavu katika eneo la kijiji hicho kwa ajili ya kuuza kwa wafanyabihara wanatoka inchi jirani,ambapo pia imeelezwa kuwa watoto wane kati ya hao wanatoka katika familia moja.

Mmoja wa wazazi wa marehemu Frank Robert(35) alieleza kuwa marehemu hao walikuwa wamehiti darasa la saba September mwaka huu na walikuwa wakiokota vyuma chakavu kwa ajili ya kuuza

“jana hao wanangu ambao ni mrehemu wana kitu kama kidumu asubuhi walikuwa wanakusanya vyuma vyao kwenda kuuza ndio ghafra nilisikia mlipuko mkubwa”alisema Robert.

Kwa upande wake Ruteni Col Benedict Kitenga ambaye ni mkuu wa wilaya ya kyerwa na mtaalamu wa kutegua mabomu amekili vifo hivyo kusababishwa na bomu(defencive hand grunet)ambapo amewataka wananchi kuwa na tahadhari wanapoona kitu ambacho si cha kawaida katika maeneo yao.
Kitenga alisema wilaya za karagwe na kyerwa zikom mpakani na nchi za Rwanda,Burundi,Uganda na kongo,kuwa wananchi wajihadhari na wageni wanaoingia ili kulinda amani ya nchi yao na maisha yao.

No comments:

Post a Comment