Na: JUHUDI FELIX NGARA
Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa katika wilaya ya Ngara
mkoani kagera wamelaani mauaji ya raia mmmoja na
polisi wawili wa kikosi cha usalama barabarani
na kusababisha taflani kubwa ndani ya jamii kwa kukumbwa na hofu ya ya
kushindwa kuliamini jeshi la polisi katika utendaji wake wa kazi ya
kulinda raia na mali zao.
Katibu mwenezi wa CCM wilayani Ngara Pastori Damiani aliliambia gazeti hili jana kuwa
jeshi la polisi linatumia nguvu katika utendaji kazi zao na kusababisha wananchi
kushindwa kulithamini kama ni chombo cha dola
Damiani alisema kuwa serikali pamoja na kuliamini jeshi la
polisi kufanya kazi za kulinda raia na mali zao bado jeshi hilo linawanyanyasa
raia na kutumia nguvu kwa wavunjaji wa sheria kwa kuwadai rushwa
Alisema mauaji ya raia wa kata ya mugoma na wananchi kuua
askari polisi kasha kukiunguza kituo cha polisi Desemba 15 siku ya gulio yalisababishwa na askari hao kutumia nguvu nyingi kwa raia
huyokutaka kuchukua pikipiki iliyokuwa gereji kwa nguvu kabla ya kumaliza
matengenezo na kuikabidhi kwa mteja wake.
“Kama wangeandika maelezo ya makosa ya pikipiki na namba
zake kasha wakatoa agizo la mmiliki kufika polisi aidha kituo cha Mugoma au
makao makuu wilayani kasha kuendelea na shughuli zao mauaji yasingelitokea”.Alisema
Katibu Mwenezi
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha NCCR -Mageuzi
Staford Festo alisema kutokana na mauaji hayo serikali haina budi kujifunza kwa
matukio ya mauaji yanayofanywa na jeshi la polisi nchini kwa kukiuka ibara ya
14 ya Katiba ya nchi ya isemayo kila raia ana haki ya kuishi .
Festo alisema kuwa
kitendo cha kuendelea na na mauaji kwa jeshi la polisi kukiuka miiko yao ya kazi
ni kusababisha imani ya wananchi kuidharau serikali kwa kuwa haichukui hatua za
kinidhamu kwa chombo cha dola kilichopewa mamlaka ya kulinda usalama wa raia
Aliongeza kuwa wananchi licha ya kutumia nguvu na rasilimali
zao kujenga kituo cha polisi katika kata mbalimbali wilayani ngara bado
wanakasirishwa na unyanyasaji wa vyombo vya dola kukandamiza haki zao
“Kinachosikitisha ni askari hao kufuata wananchi siku za
magulio nyakati za kukaribia sikukuu na kudai rushwa kwa nguvu hasa wanapokamata vyombo
vya usafiri kubainika na makosa au kuviendesha bila kuwa na leseni.Alisema
Wakati huo huo mchambuzi wa masuala ya kijamii wilayani
Ngara na ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la HDT Dr Peter Bujari alishauri kuundwa
kwa kamati huru ya uchunguzi wa mauaji bila kuhusisha polisi wanaotuhumiwa kuwa
chanzo cha tatizo ili haki itendeke na sheria ichukue mkondo wake
Alisema mkuu wa wilaya ya Ngara costantine kanyasu na mkuu
wa jeshi la polisi nchini IGP Saidi Mwemawahakikishe wanahusisha watu maarufu
wa kisiasa kidini na kijamii katika kupata ukweli wa mienendo ya utendaji kazi
wa polisi na matumizi ya vyeo walivyo navyo katika kulinda raia na mali zao
Aidha Dr Bujali alisema kamati ya uchunguzi ikikamilika itolewe taarifa kwa umma kuhusiana namaamuzi
yaliyopendekezwa ili kuondoa manunguniko ya wananchi kulalamikia serikali yao
kiutendaji na kutimiza wajibu wake
Alisema wilayani Ngara matukio ya unyanyasaji wa jeshi la
polisi kwa raia yamekuwa ya mazoea hasa kwa kipindi cha uongozi wa mkuu wa
wilaya Costantine Kanyasu kwani hivi karibuni askari mmoja alimpiga dereva wa gari la kubeba abiria na kumsababishia
maumivu na kulazwa hospitali ya Nyamiaga kwa siku kadhaa.
Hata hivyo mbunge wa jimbo la Ngara kupitia CCM Deogratias Ntukamazina ametuma salamu za rambi rambi kwa
wananchi wa Ngara na kulaani mauaji hayo ya askari wawili wa polisi na raia
mmoja kwa kujichukulia sheria mkononi.
Ntukamazina alisema licha ya kuwa jijini Dares- Salaam kikazi
anaungana na wananchi wa ngara kwa maombolezo na kwamba viongozi wa serikali wafanye uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha
kuhatarisha amani wilayani Ngara.
No comments:
Post a Comment