Na
JUHUDI FELIX
RUGU-KARAGWE
Askari wawili wa jeshi la polisi wilayani Ngara
wameuwawa katika kijiji cha Kasheshe kata ya Rugu wilayani Karagwe
kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa meno saba ya tembo yenye uzito wa kilogramu 34 kutoka katani humo.
Askari hao wakiwa na gari aina ya Noha namba
hazitambulika kutokana na gari hilo kuchomwa moto na wananchi wenye
hasira, walitokea wilaya ya Ngara wakiwa
na mpango na wa kununua meno hayo kutoka kwa watu ambao hawajajulikana kuwauzia
meno hayo.
Wananchi walifunga barabara zote zinazotoka kijijini
hapo na kufanikiwa kulikamata gari hilo, na kuanza kuwapa kipigo hadi maaskari
wawili kufa hapo hapo na mmoja ambaye amejulikana kwa jina moja la Braightoni kufanikiwa kutoroka na kujiasalimisha kituo
kidogo cha polisi Kyanyamisa akiwa na silaha.
Wananchi hao waliweza kuwashambulia watuhumiwa
na kisha gari walilokuwa nalo kuteketezwa kwa moto jambo
lililopelekea maaskari hao wawili kupoteza maisha.
Askari hao
waliouwawa walijulikana kwa majina ya E1446 Sajenti Thomasi Magiro
na E 8889 Koplo Damasi Kisheke wote kutoka katika kituo cha polisi
cha wilaya ya Ngara, ambapo pia askari mwingine ambaye amejulikana kwa jina
moja la Braighitoni aliweza kuwatoroka wananchi hao na kujisalimisha katika
kituo cha polisi Kyanyamisa.
Mganga mfawidhi
wa hospitali teule ya Nyakahanga wilaya ya Karagwe Dr Andrew
Cesari amedhibitisha kupokea miili ya marehemu hao na alisema
kuwa uchunguzi wa kitabibu umebainisha kuwa vifo vya marehemu hao vilitokana na
kipigo kikali kilichosababisha majeraha ya kuvuja damu nyingi na
kupelekea mauti hayo.
Kamanda wa jeshi
la polisi mkoa wa Kagera Philipo Kalangi amefika katika eneo la tukio na
kuthibitisha kuwa waliouwawa ni askari amesema kuwa uchunguzi unaendelea wa
kubaini shughuli ilikuwa imewaleta askari hao na chanzo cha vifo vyao pia
amewataka wananchi kutojichukulia sheria mikononi kama ambavyo hapa anaeleza wakati akiongea na
wananchi.
No comments:
Post a Comment