NA
JUHUDI FELIX
KAYANGA-KARAGWE
Baada ya
tukio la askari wawili wa jeshi la polisi kutokea wilayani Ngara kuwawa na wananchi katika kijiji cha
Kasheshe katani Rugu wilaya ya Karagwe kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya
ujambazi wananchi wameonesha kukerwa na upotoshwaji wa taarifa zilizotolewa na
vyombo vya habari vya nje ya mkoa wa Kagera.
Wakichangia
mada katika kipindi kilichorushwa na vituo vya Redio Fadeco fm na Redio Kwaragwe vyote vya hapa wilayani wananchi hao walisema kuwa
imefikia hatua vyombo hivyo viache kundanya umma kwani kuficha ukweli huo na
kuendelea kutetea maovu sio njia sahihi
ya kutatua tatizo bali ni kuweza kutoa taarifa zilizosahihi ili kuweza kukomesa
vitendo viovu hivyo katika jamii.
Akitoa maoni na ushauri wake Sabbi Rwazo ambaye
ni diwani wa kata ya Kanoni kupitia
tiketi ya CCM akionesha kusikitishwa kwake na upotoshwaji wa habari
ulifanywa na vyombo vya nje ya mkoa huu alisema Taifa limedanganya kupitia chombo cha Umma na kuongeza kuwa amejaribu kuwatafuta kutoa ufafanuzi hawakuweza kupokea simu.
Wakionesha
kupoteza imani na jeshi la polisi hapa nchini wamesema matukio ya mauaji dhidi
ya raia yanayofanywa na jeshi hilo ndilo chanzo kinachopelekea wananchi kukosa
imani na chombo hicho chenye jukumu la
kulinda usalama wa raia na mali zao.Wamesema baadhi ya askari waliingia katika jeshi hilo huku wakiwa mwenendo wao si wa kuridhisha katika jamii amba hawakuwa waaminifu ndio wanachafua jeshilo hivyo na kulitaka jeshi hilo kujisafisha kwa kusema ukweli kama ulivyo.
Wameshauri
serikali kubadili mfumo wa utoaji wa ajira kwa jeshi la polisi kuwa majina ya watakaotaka kuajiriwa na jeshi
lolote lazima yajadiliwe na kujiridhisha
kuanzia ngazi ya jamii kwani kufanya
hivyo kutasaidia kupata watu ambao watakuwa na mwenendo mzuri katika jamii kuliko kutumia njia ambazo hazitambui
mtu vema kama ilivyo kwa sasa.
Na hapa ni
moja ya msikilizaji aliyetambulisha kwa
jina la Ahumuliza kutoka Omurisimbi kata ya Nyakahanga akitoa maoni na ushauri
wake mfumo wa kuajili vijana wanaojiunga na jeshi lolote ingelikuwa vema kujadiliwa na mikutano ya Vitongoji na vijiji wanakozaliwa maana wao ndio wanawafahamu vema kisha kamati za ulinzi za kijiji na kata zijadili ili kuwasilisha majina kwa mwenyekiti wa ulinzi na usalama wilaya.
Askari hao wawili wa jeshi la polisi waliouwawa ni wa wilayani
Ngara wameuwawa katika kijiji cha Kasheshe kata ya Rugu wilayani
Karagwe kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa meno saba ya tembo yenye
uzito wa kilogramu 34 kutoka katani humo.
Askari hao
wakiwa na gari aina ya Noha namba hazitambulika kutokana na gari hilo kuchomwa
moto na wananchi wenye hasira, walitokea wilaya ya Ngara wakiwa na mpango
wa kununua meno hayo kutoka kwa watu ambao hawajajulikana kuwauzia meno hayo.
Askari hao
waliouwawa walijulikana kwa majina ya E1446 Sajenti Thomasi Magiro
na E 8889 Koplo Damasi Kisheke wote kutoka katika kituo cha polisi
cha wilaya ya Ngara, ambapo pia askari mwingine ambaye amejulikana kwa jina
moja la Braighitoni aliweza kuwatoroka wananchi hao na kujisalimisha katika
kituo cha polisi Kyanyamisa.
Kamanda wa
jeshi la polisi mkoa wa Kagera Philipo Kalangi alifika katika eneo la tukio na
kuthibitisha kuwa waliouwawa ni askari na kusema kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea wa kubaini shughuli ilikuwa
imewaleta askari hao pia kubaini chanzo
cha vifo vyao amewataka wananchi
kutojichukulia sheria mikononi.
Ikumbukwe kuwa ni juzi tu tarehe o6.01.2013 askari wawili kutoka wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera walikamatwa wakiwa na meno ya tembo sita katika hifadhi ya Taifa Serengeti mkoani Mara wakiwa wameyapakia katika pikipiki waenda kuwauzia watu waliokuwa mjini Mugumu serengeti.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Philipo Kalangi hana budi kukaa na kamati ya ulinzi na usalama mkoa ili kujipanga upya kwa ajili ya kurejesha imani ya jeshi la polisi kwa wananchi ilikuwa imejengeka haswa kwa watangulizi wake waliofanya vizuri haswa Abdallah Msika,Tossi na wengine ambao waliweza kuimarisha ulinzi katika maeneo ya pori la Kimisi,Nyakanazi uzuri wa Kondoo na maeneo mengine mengi hapa Kagera.
No comments:
Post a Comment