Jumla
ya warembo arobaini kati ya sitini wa Miss Utalii Tanzania kutoka mikoa
yote ya Tanzania.tayali wameripoti kambini leo,kuanza kambi Taifa ya
siku 21 kuanzia leo. Kambi hiyo mwaka huu iko katika Hoteli ya
Ikondelelo Lodge iliyoko Kibamba Dar es Salaam.
Warembo walio ripoti kambini hadi sasa ni kutoka mikoa ya Arusha
(Rose Godwin), Dar es Salaam 1 (Sophia Yusuph),Dar es Salaam 2(Ivon
Stephen),Dar es Salaam 3 (Irine Thomas),Dodoma (Erica Ekibariki), Geita
(Hamisa Jabiri), Iringa (Debora Jacob), Kagera 1(Elline Bwire), Kagera2
(Jania Abdul), Kagera 3(Mulky Uda), Kilimanjaro (Anna Pogaly), Lindi
(Joan John), Mtwara (Halima Hamis),Mara (Dorine Bukoni), Manyara (Mary
C. Lita), Mbeya (Diana Joachim), Mwanza (Jesca Peter), Morogoro (Hadija
Said),Tanga (Sarafina Jackson), Tanga (Leah Makange), Tabora (Magreth
Malalle), Njombe (Pauline Mgeni), Rukwa (Anganile Rogers), Katavi (Asha
Ramadhani ), Simiyu (Flora Msangi), Shinyanga (Lightness Kituwa), Ruvuma
(Furaha Kinyunyu), Kigoma 1(Zena Ally), Kigoma 2(Rosemary Emmanuel),
Pwani (Beatrice Iddy), Singida (Neema Julius), Singida (Christina
Daud),Vyuo Vikuu (Irine Richard), Vyuo Vikuu (Hawa Nyange)
Warembo wote wakiwa kambini,watapewa mafunzo na semina mbalimbali
kuhusiana na Utalii, Utamaduni, Uwekezaji, Afya ya Jamii, Elimu ya
Jamii, Wanyama Pori, Mazingira, Madini,Ulinzi Shirikishi n.k, chini ya
jopo la wakufunzi la mashindano haya wakiongozwa na mkufunzi mkuu (Chief
Choreographer) Erasato Gideon, pamoja na Mkufunzi Mkuu wa Ngoma za
Asili Mariam A. Kweji toka Kaole Sanaa Group,Mkufunzi wa Miziki na Dansi
la Asuku Che Mundugwao,wakufunzi wa minato na miondoko ya Urembo na
Mitindo Caroline Y. Mrosso na Evamary Gamba .
Asante
No comments:
Post a Comment