Na
Juhudi Felix
UONGOZI katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera umetoa muda wa siku 30 kwa wafugaji
wenye asili ya kutoka nchini Rwanga kuondoka na Ng'ombe wao katika ardhi ya
wananchi wa wilaya hiyo kabla hatua za kuwasaka na kutaifisha mifugo
hazijachukuliwa
Kauli
hiyo imetolewa baada yasiku chache za hivi karibuni wananchi wa wilaya
hiyo kukumbwa na taharuki ya kukosa usalama kwa kuwepo
baadhi ya wafugaji wenye asili ya
Kinyarwanda na wengine kutoka katika wilaya za
mikoa ya hapa nchini wanaoingia wilayani humo kwa kuwa na ngombe wengi
kuwanyanyasa wa zalendo wenye ngombe wachache na kuharibu mazao ya
wananchi na mazingira kwa ujumla
Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani
Kagera Costantine Kanyasu alitoa kauli hiyo jana katika kikao chake na wafugaji
wakubwa na wadogo wa kata za kasulo na Rusumo pamoja na viongozi wa kata hiz
katika shule ya sekondari ya Kata ya kasulo ili kuhakikisha usalama wa raia na
mali zao unapatikana.
Kanyasu alisema ili
kuhakikisha amani na utulivu vinapatikana ndani ya siku 30 viongozi wa vijiji
kwa kata zote wilayani Ngara wafanye usajili upya wa kuwatambua wafugaji wageni
toka nje ya vijiji vyao na mifugo waliyo nayo na kubaini walio ingia kwa njia
halali na walioingia kinyume na utaratibu wa sheria waweze kuondoka mara moja
Alisema kuwa serikali inafanya kazi
kwa maslahi ya kulinda na kutetea haki za wananchi na sio kutetea kundi dogo
lenye uwezo wa kifedha na kuwanyanyasa wachache kwani kufanya hivyo ni kukiuka
haki za binadamu na kukwepa uwajibikaji kwa mujibu wa sharia
Alisema kuwa wahamiaji haramu hata
kama walipata vibali vya kuingiza mifugo na muda wao kuisha lazima waondoke na
wengi wao zaidi ya asilimia 70 wanaingia kwa mianya ya rushwa kutokana na
watendaji wa idara za uhamiaji kufanya kazi bila uadilifu na kwamba kama bado
kuna wanaokumbatiwa na wenyeji kamati ya ulinzi na usalama itawasaka na kubomoa
makazi yaliyoko kwenye ardhi ya wanachi
ili kulinda mazingira
“Tumechoshwa na kubembelezana na
wafugaji wanaojionesha kana kwamba serikali ya Tanzania iko mifukoni mwao na
kiongozi atakayekwamisha zoezi hili lazima achukuliwe hatua haraka sana
“Alisema Kanyasu
Aidha kauli hiyo
imetolewa sanjari na kupiga marufuku
viongozi wa vijiji kuwakaribisha wahamiaji wenye mifugo kutoka ndani na nje ya
nchi wanaoomba ardhi ya kupata malisho na kusababisha uharibifu wa mazingira na
kutishia amani ya wananchi kati ya wakulima na wafugaji wilayani Ngara
Alidai kuwa wafugaji hao wamekuwa na
tabia ya kuonea wananchi kwa utajiri wao wa mifugo na kuharibu mazingira huku
wakiweka vibarua kuywachungia mifugo yao na wao kuishi nje ya wilaya au kwenye
nyumba za kulala wageni
Aliongeza kuwa baadhi ya wafugaji
kwa kushirikiana na wanachi wasio wazalendo wakiwemo baadhi ya watumishi wa
serikali wasio waaminifu wanaendesha
udalalai wa kuwaita wafugaji wengine na kuwauzia mapori ya kuchungia
bila kuhusisha wamiliki wa mapori hayo
Katika hatua
nyingine Kanyasu alisema katika kikao
hicho kuwa wafugaji wengi wanakimbiza mifugo yao kutoka wilaya ya karagwe mkoani Kagera na wilaya za
mikoa mingine hapa nchini kwa kuletwa na wanachi wasio wazalendo kwa kuwa
wameshabaini viongozi wa Ngara hawako makini katika kusimamia sheria
“Wananchi wana huruma sana katika
kukaribisha wageni lakini pia elimu ya mazingira hawajaitilia maanani na hasara
itakayopatikana kwa kuruhusu mifugo migi kuingia na kusambaza uoto wa asili”
Alisema ili kukabiliana na wimbi la
mifugo ni lazima mwenye kutuma maombi ya malisho apewe taarifa ya kumlipia
ng’ombe mmoja shilingi 12,000 /- kwa mwaka na baada ya hapo aombe upya kama
aneo litakuwepo apewe tena likikosekana aondoe mifugo yake ili kuepukana na
usumbufu kwa jamii
Baadhi ya wafugaji
waliotoa maoni yao walitofautiana kwa kudai kuwa wamepata ardhi kutoka kwa
viongozi wa vijiji na wengine kununua kutoka kwa wanachi lakini wanashangazwa
kuona tangu waingie wilayani Ngara mwakan 2002
sasa waamuliwe kuondoka
Aidha mmoja wa wafugaji hao Amabilis
Episphori alisema katika kupata maeneo ya kuchungia mifugo yao tangu mwaka
2002 walitoa fedha katika vijiji vya
kata hizo kuendesha zoezi la kutenga maeneo ya wafugaji katika mapori yaliyokuwa
hifadhi ya wakimbizi wa Kinyarwanda 1994 hadi 1996
Episphori alisema kuwa kila mfugaji
alitoa fedha kati ya shilingi 2,000 na Tsh 3,000 na kupatiwa risiti na
mihtasari ya kijiji iliandikwa na wao kupewa nakala kulisha mifugo yao katika
maeneo hayo
Kwa upande wake
Eustachius Sabasi amesema ili kuhakikisha amani ya wanachi inapatikana kati ya
wakulima na wafugaji na kuondoleana vitisho idadi ya ngombe kwa kila mfugaji
ipungue na kubaki kati ya 300 au 400 na watakao baki wapelekwe wilaya nyingine
tofauti na wilayani Ngara
“Mheshimiwa mkuu wa wilaya
kinachosumbua hapa ni viongozi wa ngazi zote kuanzia kitongoji hadi wilaya na
idara zake zinazohusika na ardhi mifugo na uhamiaji wanaendekeza rushwa
vinginevyo wafugaji wa kigeni leo waondoke tupate amani na mali zetu’ Alisema
Sabasi
Wafugaji wengine wamependekeza
kulisha mifugo kwa kuilipia shilingi 2000 kila mwaka pamoja na kulipia maeneo
ya kuchungia kati ya ekari 10 hadi 15 kwa mwaka shilingi laki moja kwa kila
mwenye ngombe zaidi ya 200 na fedha hizo ziwe za miradi ya maendeleo ya kijiji
wazo lililopingwa vikali katika kikao hicho
Hata hivyo mwanasheria
wa halmashauri ya wilaya ya Ngara na wakili wa kujitegemea Sauli Wilson
alifafanua kuwa katika sheria ya ardhi ya mwaka 1999 hakuna aliye na mamlaka ya
kugawa ardhi zaidi ya ekari 50 kijijini
kwani zaidi ya ekari hizo lazima kupata
kibali kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Wilson alisema wanaohitaji ardhi kwa
shughuli yoyote lazima kufuata taratibu za kutuma maombi katika serikali za
vijiji na kujadiliwa kasha mkutano mkuu wa kijiji kukubali ama kukataa kutokana
na sifa ya muombajina kiwango cha ardhi kama kinatosheleza wananchi katika
mipango matumizi ya maendeleo
“Kama mwenye kuomba ardhi na akapewa
kasha akaitelekeza bila kuitumia kwa malengo ya maombi yake wananchi wanayo
haki kuidai na kuitumia kwa malengo mengine ya maendeleo kwa kumnyanganya
aliyepewa bila kusababisha uvunjifu wa mamani bali kwa kufuata taratibu”
Alisema wananchi wanaharibu
mazingira kwa makusudi na kwa mujibu wa sheria ya NEMC wanatakiwa kutozwa faini
isiyopungua milioni 50 hivyo wakulima na wafugaji wawe makini ikiwa ni pamoja
na kulinda hifadhi ya wanyama pori na rasilimali zilizoko kwenye hifadhi hizo
Viongozi hao walifikia tamati ya
kikao kwa kauli moja ya kila mfugaji kuwa na ng’ombe wasiozidi 400 na kuacha vitendo vya kutishiana hatimaye
kuhatarisha usalama wa wananchi kwa
kutumia uwezo waomkubwa kiuchumi
kunyanyasa wanyonge kwa kuwatishia kufungua kesi mahakamani.
No comments:
Post a Comment