Monday, January 7, 2013

ZIARA YA MKUU WA MKOA KUKAGUA MIRADI KARAGWE



 NA
      JUHUDI  FELIX

KAYANGA-KARAGWE

Mkuu wa mkoa wa Kagera kanali Fabian Massawe anatarajia kufanya ziara  ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Karagwe  tarehe 8.01.2013
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na  katibu tawala wa wilaya ya KaragweMustafa S.Saidi imebainisha kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera atawasili hapa wilayani  tarehe 8.01.2013 na kutembelea miradi ya maendeleo mbalimbali.
Katika  ratiba ya ziara hiyo mkuu wa mkoa ataweza kupokea  taarifa fupi ya wilaya,kutembelea shule ya sekondari Ndama kukagua ujenzi wa maabara,kukagua mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Bujara,kukagua mradi wa maji Charuha , kukagua mradi wa ujenzi wa chuo cha ualimu Karagwe  kukagua  miradi mbalimbali ya kituo cha  Mavuno.

Miradi mingine atakayotembelea ni pamoja na ujenzi wa bweni la wasichana  katika shule ya sekondari Kiruruma,kukagua  kituo cha walemavu Chabalisa na kukagua ukamilishaji wa mradi wa ujenzi wa zahanati ya Omurusimbi.
Pia katika taarifa hii ya ziara ya mkuu wa mkoa wa Kagera inaonesha kuwa ataendelea na ziara  katika wilaya ya Kyerwa mnamo tarehe 9.01.2013.

No comments:

Post a Comment