Wednesday, January 6, 2016
ABIRIA WA MV SERENGETI KUTOKA BUKOBA KUELEKEA MWANZA WARUDISHIWA NAULI ZAO NA MELI YAONDOKA NA MIZIGO TU.
Abiria waliokuwa wasafiri na jioni ya leo kwa meli ya Mv Sengeti kutoka mji wa Bukoba kwenda Jijini Mwanza wamerudishiwa Nauli zao baada ya kubainika injini iliyoharibiwa na nyavu za wavuvi inahitaji matengenezo makubwa ikiwa jijini Mwanza.
Ofisa Mfawidhi wa SUMATRA mkoa wa Kagera Patrick Machia amesema meli hiyo iliyoondoka jioni ya leo kwenda jijini Mwanza ikiwa na shehena ya mizigo pekee.
Kuharibika kwa MV Serengeti kuna fanya huduma za meli kutokuwepo kati ya Mwanza na mji wa Bukoba kwasababu meli ya Mv Victoria ina kipindi kirefu imeharibika na wananchi kwenye kampeini za uchaguzi wa mwaka 2010 Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliwahaidi meli mpya na katika kampeini za mwaka 2015 walihaidiwa meli mpya sasa ni wakati wakutatua changamoto hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment