Baraza Kuu la Jumuia ya
wazazi ya chama cha Mapinduzi CCM Imewafikisha mahakamani wakuu wa shule zake
tatu za sekondari a,mbazo ni Tegeta
,Tabata na Mwembe two ya Mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa Taifa ya
jumuia ya Wazazi Abdallah Bulembo amesema wanatuhumiwa kwa ubadhilifu wa zaid ya
shilingi bilioni 2.8,huku Baraza pia likibaini matatizo makubwa katika
uendeshaji wa shule 15 inazozimilikiwa na Jumuia hiyo .
Amesema uamuzi huo wa
kufikishwa mahakamani kumefikiwa kufuatia ukaguzi uliofanywa na kubaini
matumizi mabaya ya Fedha ambayo haiendani na hesabu
za shule hizo.
Aidha amebainisha kuwa hali
ni mbaya katika shule mbili ambazo hakutaka kuziweka wazi ili kujilidhisha
kwanza kabla ya kuwabuluza wakuu wake mahakamani.
No comments:
Post a Comment