Mkoa wa Kagera tayari
umepokea shilingi milioni 810,157,000 kutekeleza sera ya elimu bure kwa shule
za msingi na sekondari kutoka serikali kuu na tayari fedha hizo zimeishaingizwa
kwenye akaunti za shule zote za msingi 888 na sekondari 190 za serikali kwa
kila halmashauri katika wilaya saba za mkoa wa Kagera.
Hayo yalisemwa na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila katika Mkutano na vyombo vya
habari uliofanyika Januari 11, 2016
Katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera alipotoa ufafanuzi wa mgawanyo wa fedha zilizoletwa katika mkoa mzima na na
jinsi zilivyogawiwa katika kila Halmashauri ya Wilaya mpaka shuleni za msingi
na sekondari kwa ajili ya kutekeleza sera ya elimu bure.
Akitoa ufafanuzi wa fedha
zilizoletwa Mkoani Kagera Bw. Mnambila alisema shilingi 309,461,000/= zimepelekwa
katika shule za msingi 888 ambapo shule 16 kati ya hizo ni shule maalum. Fedha zilizotajwa hapo juu ni ruzuku ya
uendeshaji (capitation grant) kwa kila shule ambapo kila mwanafunzi ametengewa
shilingi 10,000/= kwa mwaka, lakini fedha hizo hazikutolewa kila mwanafunzi katika awamu hii.
Vile vile zimetengwa pia
fedha za chakula kwa shule maalum 16 za msingi katika mkoa. Akitolea ufafanuzi
wa shule maalum na shule za kawaida Bw. Mnambila alisema shule ya Kashalala
iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ni ya kawaida na tayari imepewa
shilingi 354,000/= zilizopo Benki ya NMB Kayanga.
Shule ya Mgeza Mseto ni
shule maalum iliyopo katika Manispaa ya Bukoba pia nayo imewekewa shilingi
7,728,000/= katika akaunti yake ya NMB Bukoba, shilingi 3,042,000/= ikiwa ni ruzuku ya
uendeshaji aidha shilingi 7,386,000/= ni fedha ya chakula kwa wanafunzi waliopo
katika shule hiyo maalum.
Kwa upande wa shule za sekondari
za serikali mkoa una jumla ya shule 190 kati ya hizo 17 ni za bweni na shule
zote zimepewa fedha kwa ajili ya chakula
shilingi 1,500/= kwa kila mwanafunzi kwa
shule za bweni, na Serikali imetoa fedha za fidia za ada kwa shule za kutwa
shilingi 20,000/= na shilingi 70,000/= kwa shule za bweni. Vilevile imetoa
shilingi 25,000/= kwa kila mwanafunzi kwa mwaka kama ruzuku ya uedeshaji.
Kwa uthibitisho wa fedha kupokelewa shuleni Bw. Mnambila alitoa mfano
wa shule ya kutwa ya Nemba iliyopo Wilayani Biharamulo kuwa tayari imepokea
shilingi 630,000/= kwa ajili ya ada, shilingi 602,000/=kwa ajili ya ruzuku ya
uendeshaji, jumla shule hiyo imepokea shilingi 1,232,000/= kupitia akaunti yake
ya NMB Biharamulo.
Kwa shule za bweni, shule ya
Sekondari ya Rugambwa iliyopo Manispaa ya Bukoba imepokea shilingi 31,179,000/=
kwaajili ya chakula, shilingi 4,897,000/= kwa ajili ya fidia ya ada, na
shilingi 1,535,000/= kwa ajili ya ruzuku ya uendeshaji , julma shule hiyo tayari imepokea shilingi 37,611,000/= kwenye akaunti
yake ya NMB Bukoba.
Mwongozo wa Matumizi ya
Fedha
Kwa shule za Msingi,
Fedha za ruzuku ya uendashiji zitumike kununulia vifaa vya kufundishia na
kujifuzia lakini isiwe zaidi ya asilimia 30% ya fedha za ruzuku ya uendeshaji.
Asilimia 30% ya fedha hizo pia itumike katika ukarabati mdogomdogo, asilimia
20% itumike katika mitihani na uendelezaji wawanafunzi na mwisho asilimia 10%
ya fedha za ruzuku ya uendeshaji itumike katika mambo ya utawala shuleni.
Shule
za Sekondari, Fidia ya ada ambayo serikali imetoa kwa kila
shule badala ya wazazi kuitoa itumike kugharamia mambo ya jumla ya uendeshaji
wa ofisi mfano vitambulisho, shajala, mandalio ya somo, ulinzi shuleni, madawa
shuleni , uendeshaji wa taaluma( chaki, manila karatasi, michezo, mitihani ya
uendelezaji wa wanafunzi mfano majaribi o ya wiki, na mitihani ya moko).
Wito,
Katibu Tawala Bw. Mnambila alitoa wito kwa Walimu Wakuu wa shule za msingi na
Wakuu wa shule za sekondari kuzingatia miongozo ya matumizi ya fedha hizo
kwa kufuata maelekezo ya serikali na
kuacha kuyadharau kama baadhi ya yao ambao bado hawataki kuyafuata ambapo
alitangza kumvua ualimu Mkuu wa Shule Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bilele
Siasa Phocus ambaye ameendelea kutoa fomu yenye gharama kwa wazazi wa wanafunzi
wanaojiunga kidato cha kwanza na kusema kuwa maelekezo ya serikali hayatambui.
Mgawanyo wa Fedha kwa kila
Halmashauri
Kwa
shule za sekondari Halmashauri ya Biharamulo
imepata shilingi 76,525,000/=, Bukoba shilingi 56,462,000/=, Bukoba
Manispaa shilingi 122,597,000/=, Karagwe shilingi 39,639,000/=, Kyerwa shilingi
21, 403,000/=, Missenyi shilingi 29, 833,000/=, Muleba shilingi 93,757,000/=,
Ngara shilingi 60,480,000/=
Kwa shule za msingi Halmashauri ya Biharamulo imepata shilingi 43,161,000/=, Bukoba
shilingi 36,704,000/=, Bukoba Manispaa shilingi 27,385,000/=, Karagwe shilingi 37,515,000/=,
Kyerwa shilingi 37,967,000/=, Missenyi shilingi 20,115,000/=, Muleba shilingi 69,219,000/=,
Ngara shilingi 37,397,000/=
No comments:
Post a Comment