Tuesday, January 19, 2016

JESHI LA POLISI LAWASAKA MAHABUSU WATATU WALIOVUNJA GEREZA LA WILAYA NA KUTOROKA.




Mahabusu watatu waliokuwa wanashikiliwa  katika Gereza la Wilaya ya Karagwe Mjini Kayanga, wakituhumiwa kwa Makosa Sugu ya ujambazi, Wanatafutwa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Karagwe kwa Kuvunja dirisha la Gereza na kutoroka kwa kukimbilia kusikojulikana..


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya Karagwe Mika Makanja  akizungumuza na Chombo hiki ofisini kwake  kuhusiana na Kutoroka kwa watuhumiwa hao katika Gereza hilo.

Aidha, Makanja amewataja watuhumiwa hao Waliotoroka kuwa ni Mbaraka Muhamudu Mwenye umri wa miaka 38, Murushid Athumani miaka 25 na Muhindini Mtasigwa miaka 35 ambao wote kwa pamoja walikuwa wanahukumiwa kwa makosa ya ujambazi.

Pia ameongeza kuwa watuhimiwa hao walitoloka Januari 11 mwaka huu kwa kukata nondo ya dirisha la choo na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi watakapo waona watuhumiwa hao, kwakua ni watu hatari katika jamii.

No comments:

Post a Comment