KYERWA
Kikao cha baraza la madiwani wilaya ya Kyerwa kimepitisha bajeti ya mwaka 2014/2015 kiasi cha shilingi billion 20 milion 376,mia tisa tisini na tano elfu, mia tatu tisini na nne na senti 24 ikiwa haihusishi mishahara ya watumishi.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa halmahauri ya wilaya ya Kyerwa Kashunju Runyogote wakati akiongea na waandishi wa habari mara tu baada ya kupitisha makadirio ya bajeti hiyo.
Akitoa mchanganuo wa bajeti hiyo amesema kuwa mapato ya ndani ni shilingi Bilioni 2,milioni mia tano sabini na nane,mia nane hamsini na tatu elfu,mia sita na tano na senti 24 ikiwa ni asilimia 13 ya mapato yote, matumizi mengineyo ni bilioni 3,milioni mia moja ishirini na nane,hamsini elfu, mia nane kumi na moja huku miradi ya maendeleo ikiwa ni shilingi bilioni kumi na nne, milioni sabini na mia tisa sabini na nane elfu.
Amesema kuwa wananchi wa wilaya ya Kyerwa wajipange sawa sawa ili kuwezesha miradi kukamilika kwa wakati kwani miradi mingine inahitaji kuchangia kiasi cha asilimia 20 ya wananchi ili kuwezesha kama nguvu yao.
Katika hatua amesema kuwa mkakati wa halmashauri hiyo ni kupambana na uvuvi haramu katika mabwa na maziwa yanayopatikana wilayani humo na kuwataka wananchi kutekeleza azimio la kutokomeza ugonjwa wa mnyauko wa migomba na asiyefanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha,Runyogote amesema kuwa katika baraza hilo wameadhimia wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka huu kuhakikisha wanaripoti kwa muda uliopangwa.
Ameongeza kuwa wanaendelea na zoezi la utambuzi wa mifugo ambapo kila mfugo gharama yake ya kuwekewa alama ni shilingi elfu moja iliyopitishwa na baraza.
Hata hivyo amesisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kuandishwa kwenye daftari la wakazi lakini akatoa angalizo kuwa wasiokuwa watanzania hawaruhusiwi kuandikishwa kwenye daftari hilo na kusema zoezi la kuwaondoa wahamiaji haramu ni endelevu.
No comments:
Post a Comment