Wednesday, February 19, 2014

MUUNGANO KULINDWA NA KUDUMISHWA

Na
    Juhudi   Felix
Micheweni-PEMBA
Wananchi wa  Zanzibar wamesema hawako tiyari kuupinga Muungano watahakikisha wana ulinda na kuutetea kwa nguvu  zote.

 Haya yalibainishwa na mkuu wa wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othuman  Februari 06 mwaka huu katika ukumbi wa redio ya jamii  Micheweni wakati akifunga  mafunzo ya siku tano yaliyohusisha wajumbe wa bodi  wa redio za kijamii,wahasibu na mameneja wa redio zote za jamii kutoka Tanzania bara na visiwani zilizo chini ya mtandao unaofadhiliwa na shirika la UNESCO.

Mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa wananchi wa Zanzibar hawako tiyari kuvunja muungano uliopo badala yake wataulinda,kuutetea  na kuudumisha kwa gharama kwani muungano huo ni tunu na wanajua umuhimu  na faida zake za kuwepo.

Alisema kuwa wao kama Wazanzibari wananufaika mno na uwepo wa muungano na kusema kuwa  changamoto na kasoro zilizopo zifanyiwe kazi lakini haziwezi kupelekea kuuchukia muungano na kutaka kuuvunja.

Othuman alisema kuwa  kutokana na kuwepo kwa muungano  kuna wanyamwezi,wamakonde, wasukuma na makabila mengi hivi sasa yanakaa na kuishi Pemba na Zanzibar kwa ujumla bila kubughuziwa wala kuhojiwa kwani ni watanzania wote.

Aidha, alikwataka washiriki wa semina hiyo  na vyombo vya habari kwa ujumla kuhubili na kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kulinda na kutunza muungano na kuwapuuza wale wenye nia ya kutaka kuvunja muungano kwa maslahi ya binafsi.

Mafunzo  hayo ilifunguliwa na mkuu wa mkoa wa Kaskazini Dadi  Faki Dadi  pia aliwaasa washiriki hao kuendelea kutangaza na kuhamasisha wananchi juu ya kulinda na kuheshimu muungano ambao uliasisiwa   kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano.

Hata hivyo washiriki wa semina hiyo walihaidi kuendelea kuulinda na kuutetea muungano na kudumisha umoja  na mshikamano uliopo kwa sasa.

Mafunzo hayo yalikuwa mahususi kwa ajili ya kuzijengea uwezo redio za jamii zilizo chini ya shirika la UNESCO  kujitegemea  washiriki wamefundisha mchanganua wa biashara (Business  Plan) na ujasiriamali lengo ni kuwapatia mwanga na uwezo wa kujiendesha.
 

No comments:

Post a Comment