Thursday, January 14, 2016

WANANCHI WAMPONGEZA DIWANI KWA KUSHIRIKI ZOEZI LA USAFI WA VYANZO VYA MAJI,YEYE ATOA AGIZO KWA KAMATI YA MAJI.


 
Diwani  wa  Kata  ya  Ndama  Edward    Mpaka  ameitaka  kamati  ya  maji  ya  kitongoji  cha  Rwamugulusi  kuhakikisha    inasimamia  kimamilifu   huduma  ya  maji  kitongojini  hapo  pamoja  na  kuangalia  upya  uchangiaji  wa  kupata  maji  haswa  kwa  watu  ambao  wana  tape  binafsi  waweze  kuchangia   ili  kuboresha  huduma  ya  maji.

Ametoa  agizo  hilo leo  wakati  wa shughuli  za  kujitolea  kwenye  chanzo  cha  maji  ya  kitongoji  hicho  ambapo  amesema  kuwa  kuna  baadhi  ya  watu  wana tepu   zao  binafsi  lakini  haifahamiki  wanawezeshaje  huduma  hiyo  iwe  endelevu  na  wananchi  wanufaike  kwa  pamoja.



 
Mpaka  akawataka  pia  wananchi  wanaofanyashughuli  za  kibinadamu  ndani  ya  eneo  ya  hifadhi  ya  chanzo  cha  maji kuacha  mara  moja  kwani  kufanya  hivyo  ni  hatari  kwa  uhai  wa  maji pia  kuwahimizi  kuhudhuria  mikutano  wanapohitajika kufanya  hivyo.

Nao Wananchi wa  Kitongoji  hicho cha  Rwamugurusi   kata  ya  Ndama  wilayani  Karagwe  Mkoa  wa  Kagera  wameutaka  uongozi  wa  halmashari  ya  wilaya  ya  Karagwe  kupitia  Idara  ya  Maji  kushauri  kampuni  inayojenga  barabara  kwa  kiwango  cha  Lami kutoka  Kyaka  mpaka  Bugene  wilayani  hapa  kuhamisha  mtaro  wa  maji  waliouelekeza  kwenye  chanzo  cha  Maji.





 
Wakiongea  na  mwandishi wa mtandao huu  wakiwa  kwenye  chanzo  cha  maji  ambapo  walikuwa  wanajitolea  kufanya  usafi  kwenye  kisima  hicho   wamesema  kuwa  kipindi  cha  mvua  maji  yote  ya  mvua  hutiririka  na  kujaa  kisimani  humo  na  kusababisha  kuwa  machafu  sana  na  kubadilika  hadi rangi na  kuwa  mekundu.


Kwa  upande  wake  mwenyekiti  wa  Kitongoji  hicho  Thomasi   Ndyanabo   amesema malalamiko  hayo  alishayawasilisha  kwa  uongozi  wa halmashauri  na  kumuhaidi  kuwa  watayafanyia  kazi  lakini   haoni  dalili  zozote  za  kupatia  ufumbuzi  malalamiko  hayo.





 
Amesema  kwa  kipindi  hiki  cha  serikali  kupambana  na  ugonjwa  wa  Kipindupindu  ni  vema  wangelichukua  tahadhari  kubwa  kulinda  chanzo  hicho  kwani kupitia  maji  wananchi  wengi  wanaweza  kupoteza  maisha  kwani  huyatumia  kila  siku.

Akizungumzia  miundo mbinu  ya umeme  kwenye  kitongoji  hicho  ambacho  kipo  kwenye  mamlaka  ya  mji  mdogo  wa  Kayanga  mwenyekiti  huyo  alikuwa  na  haya  ya  kusema.






 
Hata hivyo  wananchi  hao  wameonesha  kushangazwa  na  kufurahishwa  na  kitendo  cha  diwani  wa  kata  hiyo  ya  Ndama kushiriki nao  kwenye  zoezi  la  usafi  wa  chanzo  cha  maji.





No comments:

Post a Comment