Wednesday, March 7, 2012
HUU MTAZAMO NI SAHII?
Tangu kuanzia tarehe 20.2.2012 nilianza ziara rasmi ya kutembelea watu wenye ulemavu katika wilaya ya ya Karagwe kwenye program hii nami ni mmoja wa watu walioko katika timu ya kuwatembelea watu wenye ulemavu.
Sasa leo hii nimekutana na moja ya mtazamo wa mtu mmoja akinena hivi USIWASAIDIE WATU WENYE ULEMAVU HASWA WA VIUNGO.sababu alizotoa ni kuwa hiyo ni adhabu kutoka mwenyezi Mungu kwa wazazi wake kutokana na makosa fulani waliyokwisha yatenda huko nyuma.Akadriki kutaja mifano akisema unakuta mtu alishawahi kuua kwasababu ya kutafuta mali au makosa mengine hivyo inakuwa ni sehemu ya chanzo cha adhabu kwa mtu mwenyewe au kutoka kwa wazazi.Je hii ni sahihi?Michango yenu ya mawazo au mitazamo yenu au wewe unayo research kama ya huyu bwana?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment