Thursday, March 15, 2012

UGONJWA WA MIGOMBA AMBAO HAUJAPATA TIBA HAPA KARAGWE.


 HILI NI MOJA YA MASHAMBA YA MIGOMBA LILILOSHAMBULIWA NA UGONJWA WA MNYAUKO BAKTERIO.

 Ugonjwa huu dalili zake migomba majani yake kuwa na rangi ya njano kwa sasa kinga iliyopo ni kutotumia panga lililotumika katika shamba lenye ugonjwa kwenda ambalo halijashambuliwa ndo ushauri kwa wananchi waliopewa na wataalum wa kilimo wilayani hapa.
Mpaka sasa wananchi haswa wa maeneo ya wilaya mpya ya Kyerwa hawajui nini hatma ya mashamba yao ya migomba ambapo ndizi ni chakula kikuu cha wakazi wa Karagwe  baada ya kukumbwa na ugonjwa wa Mnyauko bacteria mpaka sasa haujapata suluhisho ama tiba mbadala na kuendeleza mashaka mengi kwa wakulima wa wilaya ya Karagwe.Ndugu zangu na marafiki wa Karagwe nini maoni yenu na ushauri wenu kwa wanakaragwe kuhusiana na hili gonjwa na migomba.
Tunasubiria ushauri wenu na maoni yenu kwa ujumla kunusuru hali hii.

No comments:

Post a Comment