Monday, April 23, 2012

NGARA NAO KWA VISU HAYA WE MWENYEKITI WA BAVICHA WILAYA UMEMFANYA NINI MKEO?


Mwenyekiti  wa Vijana CHADEMA wilayani  Ngara korokoroni kwa kujeruhi mkewe kwa kisu
Na Shaaban Ndyamukama  Ngara
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana kupitia Chama cha Demikrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw Nestori Mashishanga anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo kwa kumjeruhi mke wake kwa kisu kwa kile kinachoelezwa kuwa ni  wivu wa mapenzi
Bw  Mashishanga alifanya tukio hilo ijumaa aprili 20 katika mji wa Rulenge wilayani Ngara majira ya saa tano usiku baada ya kumkuta mkewe jirani na baa ya Upendo kwa dada yake na kuanza kumshambulia kwa kisu kilichomjeruhi pafu la kulia na sehemu ya bega la kushoto
Kaimu mganga mkuu wa Hospitali ya Misheni ya Rulenge Dr prosper Malya alisema mwanamke huyo alipofikishwa hospitalini alilazwana alipewa matibabu ya majeraha aliyokuwa nayo kwa kushonwa sehemu alikojeruhiwa kwa kisu lakini hali ilibadilika kesho yake baada ya kushindwa kupumua
Dr Malya alisema kuwa katika kufanya zaidi uchunguzi walikuta damu imevimbia ndani ya pafu lililopatwa na jeraha la kisu na kulazimika kumfanyia upasuaji ili kuona kama damu hiyo inaweza kutoka na kuokoa maisha yake na kwa kuwa ni mapema analazimika kulala na baadaye kufanya mazoezi ya kutembea ili damu iweze kuzunguka mwili mzima
Akieleza tukio hilo katika wodi namba 5 ya Hospitali ya Misheni Rulenge mke wa Kiongozi huyo Bi Neema Nassibu miaka 24 alisema kuwa alikuwa mtaa wa Upendo kumsaidia dada yake shughuli mbalimbali na alikutwa na mumewe saa 12 jioni na hakuondoka hadi nyakati za kulala alipoanzisha fujo za kutaka arudi naye kwake kitongoji cha Murutambikwa kijiji hicho cha Rulenge
Alisema kuwa kwa kuwa hawakuwa na maelewano ndani ya nyumba na ni siku nyingi ameshindwa kuishi naye kwa ustaarabu alimkatalia na ndipo alianza kumshambulia huku akitoa kisu chake cha kukunja na kuanza kumchoma sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makubwa “Kusema ukweli mume huyu nimekuwa naye miaka mitano lakini ananinyanyasa nimemkuta na watoto wawili wa nje ya ndoa na mmoja ninamlea lakini tangu tuoane ameshakuwa na watoto watatu tofauti na ndoa yetu na hana uvumilivu kwa kuwa mimi sijajaliwa kuzaa naye”.AlisemaNeema


Mke wa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Wilayani Ngara Bi Neema Nassibu (24) akiwa wodini private chumba  namba tano  akitibiwa jeraha baada ya kuchomwa kisu na mumewe kwa kile kilichoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi
Aidha alidai kuwa katika kuangushana na kupiga kelele alikuja dada yake na shemeji yake pamoja na mfanyakazi wa baa kuingilia kati vurugu zao na hatimaye kumkamata hatimaye kumkimbiza katika hospitali kwa lengo la kupata matibabu
Alisema kabla ya tukio katika maisha yao ya unyumba wamekuwa na vurugu za kila mara kuhusu kutoaminiana katika ndoa kila mmoja akimtuhumu mwenzake lakini mumewe amekuwa akijulikana kwa kukutwa na wake aliozaa nao na wengine wa pembeni na kumtesa katika familia yao
Wanandoa hao walioana mmoja wao( Neema )akiwa kidato cha tatu na kuacha shule huku kijana huyo akiwa anafanya kazi katika mgodi wa Kabanga Nickeli kama mlinzi na wamekuwa wote mtaa wa murutambikwa  kijiji cha Rulenge kwa maisha ya Kupanga na siku za hivi karibuni  mashishanga aliacha kazi madini na kujiunga na siasa katika Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilayani Ngara
Jeshi la polisi kituo cha Rulenge wilayani Ngara limethibitisha kumshilia mwnyekiti huyo wa  BAVICHA Nestori Mashishanga na kwamba amenyimwa mdhamana kwani anaweza kutoroka maana hali ya mkewe haijaleta matumaini kiafya atika hospitali ya Rulenge.

No comments:

Post a Comment