Friday, April 27, 2012

ULIMWENGU KATOA MAONI YAKE MWENZANGU MTANZANIA UKO WAPI?

Uandikaji Katiba mpya: Tuketi tupange kwa kuangalia masafa marefu

Na Jenerali Ulimwengu
WIKI jana nilionyesha jinsi ambavyo mahali pasipokuwa na makubaliano ya dhati mchakato wowote unaoanzishwa umo hatarini kutokamilika.
Nilionyesha jinsi ambavyo hali kama hiyo ilivyosababisha nia ya kuhamia Dodoma na kuufanya mji huo kuwa mji mkuu wa serikali, ishindwe na badala yake tukazua hali tuliyo nayo hivi sasa ya misafara isiyoisha kati ya Dodoma na Dar es Salaam.

Nina hofu kwamba hali kama hiyo imeuteka pia mchakato juu ya Katiba. Hakuna maelewano ya dhati ya kuandika Katiba mpya, lakini tunaharakisha kuingia katika mchakato wa aina fulani ambao hakuna mwenye uhakika hasa tunataka kufanya nini. Ni kama vile tunasukumwa na utashi wa kuondoa lawama kwa kusema “Ah, walitaka Katiba mpya, nasi tumewapa. Sasa wanataka nini tena?”
Inavyoelekea ni kwamba Rais wa Jamuhuri ya Muungano aliamua mwenyewe binafsi kwamba atafanya jambo kuhusu Katiba, na katika uamuzi huo hakuwa amewashirikisha mawaziri wake na wasaidizi wengine. Wasaidizi wake wakuu wamesikika wakitoa matamko yanayopishana sana na dhamira ya kuandika Katiba upya, lakini ni hao hao watakaotakiwa kuusukuma mchakato huo hadi ufikie ukingoni. Tutaraji nini kutoka kwa watu ambao tangu awali wamesema hawaoni umuhimu wa Katiba mpya?
Baadaye kidogo tulishuhudia jinsi wabunge wa chama-tawala walivyoasi dhidi ya rais wao kwa sababu walihisi kwamba alikuwa amewaacha kando na kuingia makubaliano na chama cha upinzani. Hii ikazaa hali ya kichekesho ya wabunge wa upinzani kuonekana ndio wanaomuunga mkono Rais wakati wabunge wake wakimpinga.
Katika kutulizana na kuridhiana sasa inaelekea tume itakayoundwa kuratibu maoni ya Watanzania itakuwa ni tume itakayowajumuisha watu wenye masilahi yanayosigana, na ambao watatumia muda mwingi kulumbana kuhusu maudhui ya vifungu vya Katiba, badala ya kuratibu maoni ya wananchi. Sijui huo utakuwa uratibu wa aina gani. Ipo hatari ya kweli kwa tume hii kuratibu maoni ya wajumbe wake yenyewe badala ya maoni ya wananchi.
Nilikwisha kusema huko nyuma kwamba watetezi wa chama-tawala wanaweka kigingi dhidi ya mabadiliko ya kweli ya Katiba kwa sababu wanadhani kwamba mabadiliko yatakiondoa chama hicho madarakani. Huu ni upuuzi, kama nilivyoeleza kitambo, kwani kwa Katiba hii hii iliyopo chama-tawala kinaweza kuondolewa madarakani, kama tulivyoshuhudia Tunisia, Misri na Senegal, na juzi Arumeru Mashariki.
Aidha, wapinzani nao wanaamini kwamba iwapo vifungu fulani fulani ambavyo wanaviona kama vyenye kuwakwaza, wataweza kukishinda chama-tawala na kuchukua madaraka, lakini na huu nao ni upuuzi, kwa sababu hizo nilizozidhihirisha.
Tutajiingiza katika hasara iwapo tutatumia muda mwingi na fedha nyingi kujaribu kupata faida rejereja na za muda mfupi badala ya kufanya kazi ya tafakuri ya kina na mashauriano ya dhati kuhusu mustakabali wa nchi yetu kwa karne nzima ijayo.
Hatutakiwi kufanya haraka wala hatutakiwi kufanya kazi ya zimamoto. Tuache kuenenda kwa mtindo wa watu wa mpito. Hatuendi mahali; tupo hapa milele wala hatuhamii nchi nyingine, na kwa sababu tunazaa na wana wetu watazaa, hatutakufa (kama Taifa), na kwa hiyo tunahitaji kuchukua mtazamo wa mbali na tujipe wasaa wa kuangalia mustakabali wetu na kuupanga tunavyotaka uwe kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo. Karne moja ijayo i karibu.
Wajukuu za wajukuu zetu watatuona watu wa ajabu iwapo watakachorithi kutoka kwetu itakuwa ni mipangilio ya kijanja kijanja tu, ya kuviziana na kutegana. Kumbuka, mzazi anayejifikiria yeye na tumbo lake atapanda mchicha; yule anayefikiria vizazi vijavyo atapanda mnazi.
Hata hivyo, hii haina maana kwamba hakuna mambo tunayoweza kuyafanya sasa hivi. Yapo mambo kadhaa yanayohitaji kurekebishwa na yakatupa ushindi wa haraka (quick wins) ambayo ni kero tu, wala si matatizo mazito. Yamekuwapo kwa sababu watawala wetu wamekuwa hawafikiri vyema.
Kwa mfano, yamekuwapo maoni kwamba tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Hili si suala la mjadala kwa sababu sidhani kwamba atakuwapo mtu atakayesema kwamba tunahitaji tume isiyo huru. Suala pekee hapa ni kutaka kujua maana ya tume huru na jinsi inavyopatikana, bila shaka kwa kuangalia nchi ny

No comments:

Post a Comment