Chama cha
ushirika cha kuweka
na kukopa cha
TUWAKA SACCOSS kinachoundwa na
walimu wa wilaya
ya Karagwe na
Kyerwa mkoani Kagera
kimefanikiwa kuongeza wanachama
waliojiunga na ushirika
huo na kupata
mafanikio mbalimbali ikiwa
ni pamoja na
kununua hisa katika
benki ya wali mu
na ushirika mwingine.
Hayo yamebainishwa
na mwenyekiti wa
TUWAKA SACOSS Elizabeth
Bukindu wakati akisoma
taarifa ya bodi
kwa wajumbe wa
mkutano mkuu ambao
ni wenyeviti wa
matawi wa ushirika
huo amesema wanachama
wameongezeka kutoka 295
wa mwaka 2006
wakati ushirika huo
unaanzishwa na kufikia
wanachama 1498 kwa
mwaka huu wa
2015 wanaume wakiwa
ni 972 na wanawake
526
Amesema mafanikio
mengine ya TUWAKA
SACOSS ni kununua
hisa katika benki
ya walimu zenye
thamani ya milioni
tano na Ushirika
wa Towers Coperative
Joint Enterprise nazo
za milioni tano
pia .
Bukindu amebainisha
changamoto zinazokabili ushirika
huo kuwa ni
pamoja na ucheleweshaji
wa taarifa kutoka
matawini na asilimia
60% ya wanachama kutokuwa
na sifa za
kukopesheka kwa mujibu
wa taratibu za
hazina kwa kuzingatia
kiwango cha makato
ya mwanachama.
Katika mkutano
huo wanachama wamepitisha
ukomo wa madeni
kwa mwaka 2016 kuwa
ni shilingi milioni
miambili huku matarajio
ya mtaji wa
chama unakadiriwa kuwa
shilingi bilioni moja
na nusu.
Mgeni rasmi
Afisa Tarafa ya
Bugene Nyaishozi Rozalia
John ambaye amewmwakilisha mkuu
wa wilaya ya
Karagwe Deodatus Kinawiro
ameutaka uongozi wa
TUWAKA SACOSS kuhakikisha
unatoa huduma sawa
bila ya upendeleo
wowote ili kujenga
imani kwa wanachama
pia ameagiza kufuatiilia
kwa deni wanaloidai
benki ya CRDB
kuhakisha linalipwa kabla
ya Jumanne ya wiki ijayo.
Kwa upande
wake mbunge wa
Jimbo la Karagwe
Innocent Bashungwa amewataka kuwa
na wataalamu wa
masuala ya fedha
ili kulinda mafanikio
ya TUWAKA SACCOSS
na kuwahaidi kushirikiana
nao kwa masuala
mbayo yanahusu uwakilishi
wa mbunge na
atayafikisha kunakohusika.
Hata
hivyo wajumbe wa
mkutano mkuu wamepitisha
makinisi ya mapato
na matumizi ya
ushirika huo kwa
mwaka 2016 na
wanatarajia kuanza kujenga
ofisi yao ya
kudumu.





No comments:
Post a Comment