Picha Maktaba
Watoto wawili wa Familia Moja wa kijiji cha Kanoni Kata ya Kanoni Wilayani Karagwe Mkoani
Kagera Wamekufa Maji Desemba 21 mwaka huu
Kutokana na Ajali ya Kudumbukia
katika Dimbwi ambalo walikuwa wakichota Maji kwa ajili ya kutengenezea
Pombe.
Watoto hao wanaofahamika kwa majina ya shamila Ignatus mwenye miaka 10 ambeye pia ni
mwanafunzi wa shule ya msingi Ndama na mdogo wake Kato Ignatus mwenye miaka 7
mwanafunzi wa elimu ya malezi katika shule ya msingi Kanoni.
Baada ya
tukio hilo wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa ndani ya miaka minne watoto
sita wamefaliki dunia kwa kudumbukia
katika madibwi na visima ambavyo huchimbwa kutokana na shida ya maji iliyopo
kijijini hapo.
Aidha wananchi wa jamii ya Kanoni wameshauliwa
kufunika madibwi hayo na miti na kuacha matundu madogo kwa ajili ya kuingiza
kifaa cha kuchotea maji pekee ili kuepusha vifo vya watoto kufa maji vinavyo
zidi kutokea katika kijiji hicho.

No comments:
Post a Comment