Monday, December 28, 2015

WILAYA YA NGARA INAPOKEA WAKIMBIZI WASTANI WA 40 KWA SIKU.BOFYA HAPA


Wilaya  ya  Ngara  Mkoani  Kagera  kila  siku  inapokea  wakimbizi  wa  wastini  30   hadi  40   katika  kambi  ya  Rumasi  baada  ya  nchi  jirani  ya  Burundi   kutokuwa  na  utulivu  wa  kisiasa.
Kwa  mujibu  wa  Mkuu  wa  wilaya  ya  NGara  HONORATHA CHITANDA    wakimbizi  hao  baada  ya  kufika  kufika  idadi  ya  wakimbizi  250  husafirishwa  kwa  mabasi   hadi  kwenye  kambi  zilizopo  Mkoani  Kigoma.

Katika  hatua  nyingine  waziri  wa  Nishati  na  madini  Profesa    Sospeter   Muhongo  ameliangiza  shirika  la  Umeme  Tanzania  TANESCO    kufunga  umeme  ndani  ya  wiki  moja    katika  kituo  cha  ushuru  wa  pamoja(One  Border   Post)kilichopo  mpaka wa  Rusumo   wilayani Ngara   baada  ya  kubaini   umeme  unanunuliwa  kutoka   nchi  jirani   ya  Rwanda.

Katika  jengo  hilo  lenye  ofisi  za  forodha  ,uhamiaji, na  polisi   nguzo  za  umeme    wa  TANESCO ziko    mita   moja  ambapo  ofisa  Forodha  Mfawidhi    katika  kituo  cha  Rusumo  Laulent  Kagwebe  amesema   kuwa  makubaliano   yaliyopo  kati  ya   nchi  hizo  mbili  ni  kununua  umeme  kutoka Rwanda.

2 comments:

  1. AMANI inatakiwa irejeshwe Burundi, viongozi WA maziwa makuu wanahusika, lakini pia bado rais WA nchi hiyo ana nguvu ya kurejesha AMANI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amani nchini Burundi itadumu kuwa kitendawili kwani Rais wa nchi hiyo anathamini madaraka kuliko uhai na ustawi wa nchi yake na watu wake. Hivyo, jumuiya ya Kimataifa hasa nchi jirani wanapaswa kuangalia hilo kwa jicho la tatu.

      Delete