Zoezi la upigaji kura katika jimbo la Masasi mkoani MTWARA limeanza leo asubuhi kwa vituo kufunguliwa na wananchi kufuata utaratibu lakini katika kituo cha MSIFUNI 1 zoezi lilisimama kwa muda kutokana na chama cha wananchi CUF kumleta wakala ambaye hakuapishwa na walipohojiwa walisema aliyeapishwa ameugua na ambsye hakuapishwa alikataliwa na kuleta wa CHADEMA naye akakataliwa hivyo baadhi ya vijana ambao walikuwa wamepanga mstari wakagoma kupiga kura wakitaka mawakala wote watimie.
Msimamizi msaidizi wa uchaguzi jimbo la Masasi SHAIBU DADI amefika kituoni hapo na kuwatangazia waendelee na upigaji kura na ufumbuzi wa tatizo hilo limepatiwa jibu,katika kata ya NYASA watu hawajajitokeza kwa wingi badala yake anakuja mmoja mmoja.
Vikosi vya ulinzi na usalama vinapita mtaani na siraha za kivita vikiwemo vifaru huko Masasi mkoani Mtwara.
Majimbo ya Ludewa na Masasi wanachagua wabunge wao leo kutokana na uchaguzi huo kutofanyika oktoba 25 kwasababu ya vifo vya waliokuwa wagombe wa nafasi hizo ambo ni Dk Emmanueli Makaid wa jimbo la Masasi na Deo Filikunjombe wa Ludewa.


No comments:
Post a Comment