Friday, January 8, 2016
WACHINA WAWILI WANAOKABILIWA YA UHUJUMU UCHUMI KWA KIASI CHA BILIONI 1.1 WAACHIWA KWA DHAMANA.
Mahakama Kuu kanda ya Bukoba imekubali maombi ya dhamana ya raia wawili wa China wanaokabiliwa na kesi ya kuhujumu uchumi na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 1.1 wakati wa miundombinu ya umeme kwenye ujenzi wa barabara ya Kyaka -Bugene.
Watuhumiwa wengine wawili waliokuwa Mameneja wa TANESCO Wilaya ya Karagwe wataendelea kukaa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Januari 18 ambapo raia hao wa China hawaruhusiwi kusafiri nje ya Mkoa bila ruhusa ya Mahakama na hati zao za kusafiria zitakabidhiwa kituo cha polisi Karagwe.
Raia hao wa China wamepewa dhamana hiyo baada ya kiasi hicho cha pesa bilioni 1.1 kulipwa mahakamani hapo lakini ikaelezwa mahakamani hapo kuwa bado wanakesi ya kujibu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment