Sunday, January 3, 2016

WAFANYAKAZI WA JESHI LA MAGEREZA WASHEREKEA MWAKA MPYA KWA KUWAKUMBUKA WAHITAJI..


 Wafanyakazi  wa jeshi  la  magereza  Mkuza mjini  Kibaha  mkoani  Pwani wameadhimisha  mwaka  mpya  kwa  kuwatembelea  na  kuwafariji  watoto  yatima  na  wagonjwa waliolazwa  wodi  ya  wajawazito wazazi, na  watoto  ikiwa  ni   sehemu  ya  sadaka  yao  ya  kumshukuru  Mungu kumaliza  salama  mwaka  2015  na  kuanza  mwaka  2016





Katika  ziara  yao  hiyo wafanyakazi  hao walitoa   zawadi  mbalimbali  zikiwemo  sabuni  za  kufulia, maji  safi  ya  kunywa,mafuta  ya  kupaka  mwili,mchele, mafuta  ya  kupikia ,mbuzi, na  viatu  aina  ya  YEBOYEBO  na  bidhaa  yenye   thamani  ya  zaidi  ya  shilingi 800,000

Mkuu  wa  Gereza  la  Mkuza  Mrakibu  mwandamizi   wa  jeshi  hilo  SSP Emmanuel  Malisa  amesema  wameona  furaha  ya  mwaka  waihamishie  kwa  watu  wenye  mahitaji  kuliko  kura  na  kunywa  tu  wakati  wapo  wahitaji.

No comments:

Post a Comment