Na
JUHUDI FELIX
ADELINE BERCHMANCE
Soko Kuu la Mwanza kama yalivyo masoko mengine linajishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji ambapo moja ya shughuli hizo ni biashara ya Mama Lishe.
Soko hilo ambalo lipo katikati ya jiji la Mwanza karibu na eneo la Stendi Kuu ya zamani ya mabasi yaendayo mikoani la Miti Mirefu, Mama Lishe hutoa huduma ya chakula na vinywaji kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya soko hilo.
Wakati taasisi na wanaharakati mbalimbali wakipigania kuwepo kwa usawa wa kijinsia katika nyanja zote hali ilionekana kuwatofauti sokoni hapo baada ya kubaini biashara hii inafanywa na akina mama na kupewa jina la Mama Lishe.
Mmoja wa mama lishe hao aliyezungumza na waandishi wa makala haya Fatuma Hamis (30) alisema kuwa biashara ya chakula linachukuliwa kama biashara ya wanawake.
"Biashara hii inachukuliwa kuwa ya kina mama wanaume wanasema hawawezi kuingia jikoni kupika na kuwapakulia wanawake na wanaume wenzao, wanaichulia kama kazi ya aibu." alisema Fatuma.
Hata hivyo Fatuma alibainisha kuwa kuna baadhi ya wanaume wamebadili mtazamo huo na kwamba katika kizimba chake anakotolea huduma anafanya kazi na mwanaume ambaye shughuli yake kuu ni kukaanga samaki, kupika chapati na wakati mwingine kupiga deki pale ambapo kuna kuwa na upungufu mkubwa wa wafanyakazi ambao ni wanawake.
Deus Kilonge ndiye anayefanyakazi na Fatuma, alisema ingawa anafanya kazi na mama hao hajisikii huru kutokana na wanaume wenzake wanaofika kupata huduma mahali hapo kumbeza kwa kazi yake na hasa wakimkuta anapiga deki.
"Naifanya hii kazi kwa sababu sina kazi nyingine ya kufanya maana wenzangu hunitania sana na kuniuliza kwanini nafanya kazi za wanawake na wakati mimi ni mwanaume". Alisema Kilonge.
Hata hivyo Kilonge akikumbuka historia ya maisha yake ya kulelewa na mama yake baada ya baba yake mzazi kuwatelekeza, anabainisha hali hiyo ndiyo iliyompelekea kufanya kazi na akina mama kwani tangu utoto wake mama yake alimpa misingi ya kufanya kazi yoyote bila kubagua.
Kuhusu kuongozwa na mwanamke awapo kazini Kilonge alibainisha kuwa hana wasiwasi na suala hilo kwani yeye anachojali ni kufanya kazi na kulipwa ujira wake na hivyo kuiwezesha familia yake kiuchumi.
Huduma nyingine inayotolewa sokoni hapo na kubainika kutokuwa na usawa wa kijinsia ni biashara ya uuzaji wa nyama katika mabucha ambapo biashara hii inaonekana kufanywa na wanaume huku wanawake wakionekana kutojishughulisha na biashara hiyo kutokana na kikwazo cha mtaji.
Utafiti uliofanywa uligundua kuwa wanawake wengi ni wanunuzi wa nyama lakini si wauzaji katika mabucha, huku wanawake waliokutwa wakinunua nyama katika mabucha hayo wakisema wao hawawezi kuifanya biashara hiyo kutokana na kushindwa kukokopa fedha ya mtaji kwakukosa vigezo vya kukopeshwa.
"Biashara hii ni ya wanaume, sisi hatuwezi maana mtaji wake ni mkubwa na hatuwezi kukopa kwa sababu wanaotoa mikopo wanataka hati ya nyumba na sisi nyumba hatuna nyumba ni mwaume hata kama mmejenga pamoja". Alisema mama ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini.
Katika utafiti huu kumegundulika kuwa biashara zenye kuhitaji mtaji mkubwa hufanywa na wanaume kwasababu wana nafasi kubwa ya kupata mtaji kwa njia ya mikopo na pia jamii inapaswa kubadili mtazamo juu ya kazi na suala la jinsia ili kuweza kujikomboa na umaskini.

No comments:
Post a Comment