Na:
Mbeki Mbeki
Karagwe
Karagwe
Jumla ya wanawake 450 walio
wajane katika Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera wanakabiriwa na changamoto
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosekana msaada wa kisheria unaoweza kudai haki
zao za msingi.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na
Mwenyekiti wa umoja wa wajane katika Wilaya ya Karagwe na Kyerwa Grace
Mahumbuka wakati akizungumza na Habari Leo ofisini kwake.
Mahumbuka alisema kuwa wajane
na watoto yatima wanajishughulisha na shughuli zao mbalimbali ili kupata kipato
chao cha kukidhi ukali wa maisha, ambapo alisema huyang’anywa, hudhulumiwa,
hudhalilishwa hata kubakwa na kushindwa kupata haki zao kwa kukosa asasii ya
kisheria ya kuwasaidia.
Alisema kuwa vitendo vya
kurithiwa kwa nguvu kindoa na mashemeji zao na baadhi ya wanajamii, watoto
yatima wa kiume kulawitiwa na kuingiliwa kinyume cha maumbile kuwa vitendo
hivyo vimechangia msongamano wa mawazo katika kundi hilo
Alisema kuwa kundi la Wazee,wajane na walemavu ni makundiyanayokabiliwa na changamoto za
kutothaminiwa, kutoheshimiwa, kutosikilizwa na jamii na baadhi ya
vijana kuwa watovu wa nidhamu ndani ya familia zao na jamii inayowazungunka.
Mahumbuka alisema serikali
ilitangaza kuwa wazee wote kupatiwa matibabu bure kuwa mpaka sasa serikali
haijachukua hatua ya utekelezaji kikamilifu.
Aidha alisema Pensheni kwa
Wazee kucheleweshwa na kutolipwa kabisa na kuongeza kuwa pensheni
kwa wazee wakulima inayozungumzwa Bungeni na serikali kutotekelezeka.
Hata hivyo ameitaka serikali
kutambua haki za msingi katika makundi hayo na kuwafanya kuishi kiusalama na kulindwa kwa
mali zao ni pamoja na kupatiwa bima ya
afya kwa ajili ya afya zao.
No comments:
Post a Comment