Monday, October 1, 2012

BASI LA TEKETEA KWA MOTO,ABRIA 30 WAHOFIWA KUFARIKI DUNIA NA WENGINE 9KUJERUHIWA


Na Mbeki Mbeki
BIHARAMULO

ABIRIA kadhaa wanasadikika kufariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuteketea kwa moto katika kijiji cha Nyantakala wilayan Biharamulo mkoani Kagera.

Ajali hiyo imetokea saa 4:30 asubuhi imelihusisha basi la kampuni ya Adventure lenye namba T 294 ABD aina ya scania ambalo lilikuwa likitokea mkoani Mwanza kwenda mkoani Kigoma.

Majeruhi wa ajali wamelazwa katika hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo na kwamba kati ya majeruhi tisa wawili kati yao akiwe ajenti wa basi hilo Dotto Tryphone[30]mkazi wa Nyakanazi wamevunjika miguu wakati wakijinasua kutoka kwenye basi hilo baada ya kushika moto.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera,Philip Kalangi alithibisha kutokea kwa ajari hiyo na kusemakuwa basi hilo ni aina y nisani diseal lenye namba  T 293 BDP na kuwa chanzo cha ajari hiyo ni hitalfu ya umeme sehemu ya injini na kwamaba hakuna kifo hata kimoja isipokuwa mali za abria na basi vimeteketea kwa moto uchunguzi unaendelea,abria walionusurika  walisafirishwa na gari jingine .

Aidha Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wakiwemo majeruhi wamesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya basi hilo kufika kwenye tuta  la kuzuia mwendo kasi  walishitukia moshi unatokea ndani ya basi kabla ya kushika moto na kuanza kuteketea.

‘’Basi lilikuwa kwenye mwendo wa kawaida lakini lilipofika kwenye bamzi[tuta]tulishtukia basi linashika moto ,tukaanza kuruka,kuna baadhi ya wenzetu hasa watoto na wazee huenda wameteketea kwenye basi hilo,maana basi limewaka na kuwa majivu kabisa’’alisema Tryphone.

Akizungumzia ajali hiyo kwa shida akiwa katika wodi ya majeruhi Tryphone alisema huenda chanzo cha kulipuka kwa basi hilo kinatokana na hitilafu katika mfumo wake wa umeme.

Dereva wa basi hilo ambaye hakutambulika jina lake haijajulikana kama alikimbia au aliteketea kwenye basi hilo mara baada ya kutokea ajali hiyo. 
Mganga mkuu msaidizi wa hospitali hiyo Gabriel Mashauri amesema amepokea majeruhi tisa na kwamba saba kati yao walikuwa katika hali mbaya lakini bado wanaendelea kupatiwa matibabu.

Amewataja majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo ni Phinihas Elias[37]mwalimu wa shule ya sekondari Shamaliwa Igoma jijini Mwanza,Pius John[21],Msigwa Isaya[18]mwanafunzi wa shule ya sekondari Kigoma,Johary Chapa[23]Mkazi wa Kwimba mkoani MwanKza,Josephina Ngereza[46],Rashidi Mahonda[48] na Eles Ngereza[60] wote wakiwa wameungua moto sehemu mbalimbali za miili yao.

Waliovunjika miguu katika ajali hiyo wakati wakijinasua kutoka ndani ya basi hilo wametambulika kwa majina ya  Dotto Tryphone[30]mkazi wa Nyakanazi na Zainabu Issa ambao wote wamevunjika miguu ya kushoto.
Dk.Mashauri alisema hajapokea maiti waliotokana na ajali hiyo

No comments:

Post a Comment