Karagwe
Migogoro ya Aridhi iliyokithiri katika wilaya ya Kyerwa na Karagwe
imeelezwa kuwa chanzo chake kikubwa ni viongozi wa serikali za vijiji na
Vitongoji kugawa ardhi bila kufuata sheria ,kanuni na utaratibu.
Hayo yalibainishwa jana na mkuu wa mkoa wa kagera kanal mstaafu
Fabian Inyasi masawe wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani
humo.
Kanal Mstaafu Masawe amesema kuwa,viongozi wa serikali ya vijiji na
vitongoji wamechangia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na
wafugaji katika wilaya mbalimbali za mkoa huo ikiwemo wilaya ya karagwe na
Kyerwa ambapo migogoro hiyo imekithiri sana.
Alizitajabaadhi ya kata
zilizokithiri kwa migogoro hiyo ni
pamoja na kata ya Rugu ,Nyakasimbi Rugera na kihanga kuwa kata hizo
zinachangiwa na viongozi wa ngazi za chini.
Kauli ya mkuu wa mkoa huyo ilitokana na barua ya malalamiko kwake
kutoka kijiji cha Mililo Ruhita kata ya Rugu
ya May 29 mwaka huu iliyodai mwenyekiti wa kitongoji hicho kuwatapeli
wananchi hao zaid ya kaya 100 na kuwauzia
ardhi kinyume cha utaratibu na
bila stakabadhi kiasi cha million 50.
Kwa mujibu wa malalamiko ya wananchi hao ambao walimtaja mwenyekiti
huyo wa kitongoji kuwa ni Tiziwa Mkolelanda,walisema kuwa watanzania wanaoishi
kwenye maeneo hayo ,hutengewa ardhi kidogo ambapo eneo kubwa huuziwa
wanyarwanda kwa ajili ya malisho.
Katika hatua nyingine wananchi wa kata ya Rugera Wilayani humo
wamewalalamikia baadhi ya wananchi wapatao 12 ambao wanahusishwa na tuhuma ya
kuvamia ardhi ya kijiji na kujigawiya maeneo makubwa ukiwemo uvamizi wa ardhi unaosababishwa na
wamiliki wa Block(vitalu)
Kanali Massawe alisema kuwa waliouziwa ardhi kinyume cha utaratibu
watangolewa na kamati ya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na wananchi.
“Ardhi ni mali ya
Serikali ya kijiji hao watu waliouziwa
mbuzi kwenye gunia na walio husika ni lazima wachukuliwe hatua”Alisema
Massawe.
Aidha alisema kamati ya ulinzi na usalama haina budi kusuruhisha
migogoro hiyo na kuwa watu wa kata ya Rugu watoe ushirikiano wa dhati ili
kumaliza migogoro hiyo inayoweza kuhatarisha usalama wa Raia ambapo aliongeza
kuwa mipaka ya kata ya Rugera na wilaya ya Muleba watalamu walishatoka mkoani kusuruhisha matatizo hayo.
Hata hivyo amewataka wananchi wa kata zilizo na migogoro ya ardhi
wenyeviti wao wa vitongoji na vijiji wasichaguliwe tena maana wameshiriki kuhatarisha
migogoro katika jamii.
No comments:
Post a Comment