Karagwe
Serikali mkoani kagera imemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya
ya karagwe kuwalipa wanamgambo 52 kiasi cha shilingi million 25 walioshiriki
kudhibiti magendo ya kahawa kwenda nje
ya nchi na uvunaji wa kahawa mbichi Hayo yalisemwa jana na mkuu wa mkoa wa
kagaera kanal mstaafi Fabiani Inyasi masawe wakati alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari mkoani humo.
Kanali mstaafu Massawe alisema kuwa madai hayo ni halali
,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hana budi kuwalipa na kuwa kutowalipa
wanamgambo hao ni kitendo cha unyanyasaji,udhalilishaji,ambapo aliongeza kuwa
wilya ya karagwe na Kyerwa katika msimu
huo walipata zaid ya shilingi 200 kutokana na mauzo ya kahawa,kuwa ahaoni kwa
nini wanamgambo hao wasilipwe stahiki yao.
Alisema wananchi wa wilya hizo hawana budi kupiga marufuku magendo
ya kahawa kwenda nje ya nchi ,kwamba mauzo ya kahawa ndiyo yanasababiswa kuwepo
kwa miundo mbinu mizuri ya barabara ,huduma bora ya afya na mashule.
Aliongeza kuwa wanamgambo hao kulinda na kudhibiti kahawa ilikuwa
ni kwa maslahi ya Taifa na Halmashauri zao
na wananchi wa wilya hizo ,na kuwa ni marufuku kuendeleza vitendo vya
magendo ya kahawa katika mkoa huo na kuwa atakaye bainika anakahawa na gari
vitataifishwa na nipamoja na kufunguliwa mashtaka.
Kwa mjibu wa barua ya wanamgambo hao iliyonakirishwa kwa mkuu wa
mkoa wa kagera ya May 11 mwaka
huuwalisema kuwa walipewa kazi hiyo na Halmashauri ya wilya ya karagwe April 16
mwaka 2012 na halmashauri imeendelea kukaidi madai yao.
Walisema kuwa walifanya kazi
hiyo kwa mda wa siku 195 kwa makubaliano ya kulipwa shilingi 5000 kwa
siku,ambapo kila mwanamgambo alipaswa kulipwa kiasi cha shilingi 975,000 na kuwa hadi sasa
walilipwa kiasi cha shilingi 725,000 kwa kila mmoja.
Aidha walisema kuwa kwa malipo ya sasa ,wanamgambo hao wanadai siku 50 kwa kila mmoja zenyetahamani ya
shilingi million 25 na kuwa kwa mda mrefu
familia zao zimeishi kwenye mazingira magumu na watoto wao kurudishwa
kukosa michango mbalimbali wakati Halmashauri ikitambua deni hilo.
Hata hivyo katika barua hiyo waliendeleza kuwa,wamekuwa wakipewa
vitisho na baadhi ya viongozi wa Halmashauri na serikali kuwa vinawakatisha tama
katika shughuli za utendaji.
No comments:
Post a Comment