Saturday, September 21, 2013

UNYANYASAJI BADO TATIZO KWA JAMII YETU

Katika uchaguzi uliofanywa kuhusu unyanyasaji wa kijinsia imebainika kuwa jumla ya matukio 529 ya unyanyasaji ikiwemo kubakwa kukatwa mapanga na kupewa mimba za utotoni. Yamelipotiwa polisi katika wilaya ya Kayagwe.
 
Hayo yamesemwa na Bi Ashura kajura kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe katika mkutano wa unyanyasaji wa kijinsia katika jamii uliofanyika katika ukumbi wa Community Habilant education Management (CHAMA) uliopo omulushaka Karagwe.
 
Bi Kajuna alisema kuwa kwa miaka miwili 2011 na 2012 Jumla ya matukio 529 ya unyanyasaji kijinsia yakiwemo ya ubakaji 59 kukatwa mapanga 32 na mimba za utotoni 30 yalilipotiwa polisi katika wilaya hiyo.
 
Aliendelea kusema kuwa unyanyasaji ni udhalilishaji anaofanyiwa mtu kutokana na jinsia yake na kuwa asilimia kubwa wanaonyanyaswa ni wanawake kutokana na uonevu unaopangwa na kukubaliwa na Mila na desturi.
 
Kajura amevitaja vyanzo vya unyanyasaji kuwa ni pamoja na mila na desturi sheria ya ndoa ya kiislamu kuozwa kwa nguvu ukeketaji wa mtoto wa kike, kunyimwa haki ya kutoa maoni ya ukosefu wa Elimu kwa watoto wa kike unaowapelekea kutojiamini na kuwa katiba kuiweka wazi haki za mwanamke.
 
Kwa upande wake Aman Ndabatunga ambaye alishiriki katika mdaharo huo alisema kuwa chimbuko la tatizo la unyanyasaji wa kijinsia katika jamii ni kutokana na mfumo dume ambao siku zote ulimwona mwanamke kuwa kiumbe Taifa
 
Ndabatunga aliendelea kusema kuwa kutokana na unyanyasaji huo kuna athari nyingi ziliojitokeza katika jamii ambazo amezitaja kuwa maambukizi ya ugonjwa wa ngono, kuchoka mwili na kuzeeka kutojiamini na kuthaminiwa kutokuwa na maamuzi kusababisha ulemavu na kifo na kukuwa vifo na kuwa zaidi ya asilimia 50 ya wanawake walio katika ndoa wanabakwa na waume zao.
 
Tumeshuhudia wamanaume wakiwapa watoto wao wa kuzaa na akiamua kumchukuliwa hatua za kisheria anaambiwa hayo ni masuala ya mila na desturi hupaswi kuwaingilia ambapo watoto wanazidi kuteseka kutokana na mila na desturi zilizopitwa na wakati Alisema Ndabatunga.
 
Naye sabron kuwa mkwazi wa kitongoji cha mgaba kijiji cha Bujara anayetuhumiwa kumbebesha Mimba mwanae wa kuzaa mwenye umri wa miaka 15 mwanafunzi wa darasa la saba baada ya kufikishwa kwenye ofisi ya kijiji hicho aliojiwa kuhusu tuhuma hizo ambapo alikana kosa hilo.
 
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na mtoto ambaye anakabiliwa kuwa na ujauzito wa miezi sita alisisitiza kuwa baba yake ndiye aliyempa ujauzito huo.
 
“Tulikuwa shambani tunapalilia ndipo baba aliponitaka kimapenzi na baada ya kukataa alinishikia panga na kusema atanua na kutokana na hofu zikuweza kupiga kelele kwa kuhofia kuwa ataniua na kutokana na hofu sikuweza kupiga kelele kwa kuofia kuwa ataniua “ Alisema mtoto huyo”
 
Aliendelea kusema kuwa baada ya kuwa baada ya kurudi nyumbani hakuna lolote kwa kile alichosema kuwa aliambiwa endapo angesema chochote angeuwawa na baba yake.
 
“Niliendelea kunyamaza japo nilikuwa nahisi maumivu mwili mzima na baba aliendelea kunifanyia mapenzi mpaka akanipa mimba na nilipojisikia kuwa nina mimba niliamua kumwambia mama” Alisema mtoto huyo.
 
Kwa upande wake mama wa mtoto huyo alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kuwa baada ya kugundua  mwanae kuwa ana ujauzito alitoa taarifa kwenye ofisi ya kijji ndipo taratibu za kumkamata baba wa mtoto huyo zilifuata.
 
Aidha baada ya kukana tuhuma hizo za kumpa mimba mwanae aliachiwa huru ambapo wananchi walimfukuza kijijini humo na hatimaye kutokomea kusikojulikana.
 
Lakini Owokusima Kaihura kutoka ofisi ya ustawi wa jamii wilayani Karagwe alipoulizwa kuhusu vitendo hivyo alisema kuwa baadhi ya wazazi hawatoi taarifa za matukio hayo kutokana na uelewa mdogo walionao na kuwa wengine hukandamizwa na mila na desturi.
 
Saulo Malauri kutoka shirika la Mamas` Hope organization for legal assistance (MHOLA) alisema kuwa kuafuatia matukio hayo shirika lake aliamua kutoa huduma za kisheria  kuhusu akina mama na watoto ili kupunguza vitendo hivyo vinavyojitokeza.
 
Shirika letu lipo Bukoba na tunatoa Elimu ya Kisheria kuhusu haki za hakina mama na kwa jinsi matokeo yanavyozidi kupamba moto tumeamua kuweka ofisi zetu kila wilaya na kutua mfumo ili jamii iweze kuwa na uelewa zaidi kuhusiana na vitendo hivyo vinavyotishia amani katika jamii yetu Alisema malauri.
 
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na mwenyekiti wa asasi ya Karagwe Development Network of volunteers organization (KADENVO) Bw. Telesphory kalemela chini ya udhamin mtandao wa kufatilia sera mwanza (Initiative alisema kuwa jamii inastahili kuelimishwa juu athari za unyanyasaji ikiwa ni pamoja na kuachana na mila na desturi zilipitwa na waakti ambazo hupelea unyanyasaji huo.
 
Hata hivyo washiriki katika mdhaharo huo wametakiwa kutoa elimu katika jamii inayotuzunguka ili kuondokana na tatizo hilo ikiwezekana kutokomeza kabisa.
 

No comments:

Post a Comment