Saturday, September 21, 2013

WATAKIWA KUTOWANYANYASA NA KUWABAGUA WATU WENYE ULEMAVU

Halmashauri ya wilaya Karagwe mkoani kagera imelalamikiwa kutowajali watu wenye ulemavu wa ngozi, walemavu wa viungo, watoto yatima wakiwemo wanawake wajane yakiwa ni makundi yenye malengo yanayofanana.
 
Hayo yalisemwa jana na mwenyekiti wa umoja wa wanawake (UWK) katika wilaya ya karagwe na kyerwa Grace Mahumbuka wakati akifungua mkutano wa mabaraza ya katiba ya asasi. Taasisi na makundi ya watu wenye malengo yanayofanana.
 
Mahumbuka alisema kuwa uongozi wa Halmashauri umekuwa hauwathamini watu walio katika makundi yanayofanana huku wakiwa dhalilisha pale wanapokuwa wanahitaji msaada ikiwemo kupewa kejeli na baadhi ya viongozi wa halmashauri.
 
“Viongozi wa halmashauri wanatuchukulia kama labda sisi tulipenda tuwe hivi kama tulivyo umeshuhudia mwenyewe tulivyonyimwa ukumbi na kufukuzwa kama watoto na umeona tunavyofanyia mkutano kwenye uwanja wa michezo na ukumbi wamepewa wenye pesa” Alisema mahumbuka.
 
Alisema kwa mujibu wa kifungu cha 18(6) cha sheria ya madiliko ya kariba sura ya 83 tume imeweza kuruhusu asasi, taasisi na makundi ya watu wenye malengo yanayofanana kuandaa mikutano kutoa maoni yao juu ya rasimu ya katiba
 
Alisema katika kuziwezesha asasi taasisi na makundi ya watu wenye malengo yanayofanana kuunda mabaraza ya katiba tume imeruhusu kuendesha mkutano kuipitia barua yenye Kumb.Na. 76/386/02/150 ya julai 18 mwaka huu.
 
Alifafania kuwa tume ya mabadiliko ya kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba sura ya 83 kifungu cha (22)1 limeweka wazi upatikanaji wa wajumbe 166 kutoka katika makundi ya watu wenye malengo yanayofanana.
 
Aidha katika uchunguzi huo uliofanyika katika uwanja wa michezo wa kayanga wilayani humo Grace mahumbuka alichaguliwa kuwa  kuwakilisha kundi la wanawake wajane, Agnes Mukuta (Madhehebu), Coletha Brikmas (Walemavu wa viungo) Savela Aaron wanaishi na virusi vya UKIMWI.
 
Aliwataja wengine waliochaguliwa kuwa ni pamoja Generoza katto kundi wakulima vyama vya siasa Henerico Ernest, Neema Edward (Elimu ya juu na Brasio Stephano watu wenye ulemavu wa ngozi.
 
Naye mwenyekiti wa Halmashauri hiyo walles mashanda alikanusha tuhuma iliyoelekezwa kwake dhidi ya halmashauri yake kutowajali watu walio kwenye makundi yanaylofanana.
 
Mashanda alisema kuwa hawakuweza kupewa ukumbi kutokana na ukumbi huo kukodishwa kwa mwezi mmoja kwa asasi nyingine na kuwa umoja wa wanawake walileta maombi yao kwa kuchelewa.
 
Hata hivyo alisema kuwa halmashauri hiyo imekuwa karibu na makundi hayo akiongeza kuwa wanaykoshule ya watoto wenye ulemavu wa ngozi Kitengule walitoa ofisi ya walemavu wa viungo katika majengo yao na kuwa wamekuwa wakishirikiana na ofisi ya umoja wanawake kwa kila jambo. 

No comments:

Post a Comment