DAILY HOT NEWS
Kwa mawasiliano zaidi tumia felixjuhud@yahoo.com au +255 (0) 756 601 054
Tuesday, August 18, 2015
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 TANZANIA
Na Juhudi Felix-Karagwe
Joto la kisiasa linazidi kupanda katika jimbo la Karagwe haswa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)baada ya kuzuka hali ya sintofahamu kwa kile kuonesha kugawanyika na kuwepo mgawanyiko ndani ya chama hicho baada ya kuwepo kauli mbalimbali za kutatanisha kutoka kwa viongozi na hadi kupelekea wagombea wawili kati ya wanane waliochukua fomu na kuzirejesha kujiondoa rasmi kwenye mchakato huo wakidai ni kulinda maslahi ya chama kisigawanyike na kwenye uchagunzi mkuu wa oktoba mwaka huu.
Waliojitoa kwenye kinyanganyiro hicho wakati walikuwa wameanza kampeini za kutambulishwa kwa wanachama ni Gosbert Blandes ambaye ni mbunge anayemaliza muda wake na Karimu Amri ambaye ni Mneck wa CCM wilaya ya Karagwe.
Blandes akihojiwa na waandishi wa habari kisha kutangaza rasmi kujiondoa kwake kupitia Redio Fadeco ambayo ni ya kijamii iliyopo wilayani hapa alisema ili kunusuru chama waliona ndiyo bora zaidi kuliko kukigawanya na kuleta hali ya taharuki ndani ya chama na ikizingatia wao ndiyo wenye wafuasi wengi katika CCM hivyo waliona ni vyema wakajiondoa wote na kuwaachia makada wengine sita waliosalia kuendelea na mchakato ndani ya chama huku akisema ataendelea kuwa mshauri wa karibu na kuunga mkono mgombea yoyote yule atakayeteuliwa na chama chake.
Karimu Amri ambaye ni Mneck akitangaza uamuzi wake wa kujiondoa kwenye mchakato huo alitumia mkutano wa Jumuia ya wanawake wa CCM yaani (UWT) uliofanyika katika ukumbi wa chama hicho uliopo mjini Kayanga alisema kuwa alizingatia kauli na utaratibu uliopo kuwa Chama kwanza mtu baadae hivyo ataendelea kushirikiana bega kwa bega kuhakikisha ushindi kwa chama hicho unapatikana kwa wagombea wanaoendelea na mchakato.
Hali ilianza kujionesha kuwa ndani ya CCM wilaya ya Karagwe siyo tulivu baada ya mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Karagwe Robinsoni Mtafungwa kuitisha mkutano wa waandishi wa habari wilayani Karagwe uliofanyika kwenye ofisi za chama hicho makao makuu ya wilaya na alimshtumu sana kwa madai ya kudhalilishwa na mbunge wa jimbo la Karagwe.
Shutuma ambazo zinadaiwa kutolewa na Mbunge wa jimbo la Karagwe Gosbert Blandes dhidi ya mwenyekiti wa CCM wilaya ya Karagwe Robinsoni Mtafungwa ni kuwa alipewa shilingi milioni tatu za kuanzisha biashara ya baa hapa Kayanga,kulipiwa deni la mkopo wa milioni sita alioukopa akashindwa kuurejesha, Kupewa milioni sita na laki mbili kwa ajili ya kusimamia kesi za uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na shutuma nyingine ni kutoudhuria mkutanbo wa Blandes alioufanya katika kata ya Kiruruma Julai 17 alidai aliogopo kuabishwa kwa wanachama.
Mtafungwa amesema kuwa shutuma dhidi yake ilitokana na ziara yake aliyoifanya na Mneck wa Karagwe KARIMU AMRI katika kuimarisha chama walibainisha mapungufu na udhaifu wa mbunge kwa wanachama kwani alitoa ahadi ambazo mpaka sasa hajazitekeleza kitu ambacho alieleza inaweza kuwa mzigo kwa chama wakati wa kumnadi kwa wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alisema watu ambao walikuwa karibu na mbunge huyo wakati wa kampeini kuhakikisha anapata nafasi hiyo alisema kipindi hiki anawaona kama maadui zake wakati walimsaidia alisema yeye alikuwa kampeina wa Blandes mwaka 2010,Karimu Amri alikuwa kampeina meneja wa mbunge huyo mwaka 2005 lakini sasa wanatofauti kubwa kuliko mwaka huku.
Mtafungwa alitamka mbunge huyo kudhibitisha shutuma hizo ili kuondolea umma udhalilishaji aliotendewa yeye kama mwenyekiti wa Chama aliyechaguliwa kihalali na wanachama na kinyume cha kutofanya hivyo atachukua hatua zaidi kwa ngazi ya chama kwa kupeleka suala hilo kwenye kamati za maadili kuanzia wilaya,mkoa hadi Taifa na vyombo vingine vya kutafuta haki kama mahakamani.
Hata hivyo aliwataka wanachama wa CCM na wananchi wa kata ya Kiruruma na wilaya nzima kuendelea kuwa na imani naye na kumwamini kwani hana doa lolote na hajawahi kudhulumu cha mtu na shutuma hizo ni za mbunge kutapata kwa ajili ya kupata nafasi wakati akitambua hajatimiza ahadi ambazo alizitoa na akashindwa kuzitimiza.
Robsoni alikiri kukopa mkopo wa shilingi milioni 3 na siyo milioni 6 zinazodaiwa na Mbunge h uyo na alisema aliukopa Benki ya NMB tawi la Kayanga iliyopo mjini Kayanga wilaya Karagwe na kwa sasa anaendelea kuulipa.
Alipotafutwa mbunge anayemaliza muda wake Gosbert Blandes kuthibitisha au kukanusha madai hayo alisema hana cha kusema pia suala hilo anamwachia Mungu hivyo hawezi kuliongelea.
“Ninaomba kwa sasa jambo hili muniache nipumzike kabisaa nimewatumikia wananchi wa Karagwe kwa kipindi cha miaka 10 wanajua mabaya na mazuri niliyowafanyia wanakaragwe”Alisema Mbunge
Kujiondoa wagombea hao kumezua mminongono mingi kwa wananchi wengine wanaonesha kukubaliana na hali hiyo hivyo mchakato huo wameachiwa wagombea sita ambao ni Innocent Bashungwa,Audax Rukonge, Amoni Chakushemeire,Mwalimu Dagobart Deogratias,Kamuhangire Mjungu,na Alfred Rujwahuka ambao wanaendelea na ratiba za chama za kujitambulisha kwa wanachama na hatimae kupigiwa kura za maoni.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM wilaya ya Karagwe Robert Runyoro alithibitisha taarifa za kujiondoa kwa wagombea hao ni kweli baada ya kufuata kanuni na utaratibu zinavyoelekezwa kuwa mpaka kuandika barua kwa uongozi na walifanya hivyo na kikao cha siasa na uenezi mkoa kilifanyika na kuridhia hatua walioichukua.
Kuna taarifa zilizopo ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa wagombea hao waliondolewa na agizo toka ngazi ya Taifa kwa kile kinachoelezwa ni utovu wa nidhamu waliouonesha wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdruhaman Kinana aliyoifanya mwezi juni mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment