Na Juhudi Felix-Kyerwa
Watu watano wa familia moja katika Kitongoji cha Omukicherenje kijiji cha Mugaba Kata ya Businde wilayani Kyerwa Mkoa wa Kagera wameteketezwa kwa moto na mashamba yao yenye ukubwa wa hekali 15 na nyumba nane zimeteketezwa na vitu vilivyokuwemo ndani yake ambayo thamani yake hajajulikana baada ya kutuhumiwa kumuua mfanyabiashara wa mazao mmoja aliyekuwa amefuata mzigo wa kahawa kwenye familia hiyo.
Wakizungumza jana kwenye eneo la tukio wananchi wa kijiji hicho na wengine kutoka kwenye vijiji jirani vya kata ya Igurwa ya wilayani Karagwe walisema kuwa watu wasijulikana walipandwa na hasira baada ya kuwepo kwa taarifa za mfanyabiashara Jovinary Morandi kuwawa na kufukiwa kwenye shamba la Datusi Paulo ambaye alikuwa wakala wa mfanyabiashara huyo wa mazao na kukutwa na pikipiki ya marehemu huyo ndipo wakamtilia shaka.
Waliouwawa na wananchi hao ni Datusi Paulo Miaka (36),Lakius Paulo(30) ambao walikuwa ni wajukuu wa Henerico John miaka (70) ambaye naye aliuwawa kwenye tukio hilo la kusikitisha kwa tuhuma za kujihusisha vitendo vya kishirikina na huyo ndiye alikuwa mkuu wa familia.
Wengine waliouwawa ni Launtina Henericko (68) ambaye ni mke wa Henerico John, Sabiniani Henerico (35) na mtoto anayedhaniwa kuteketea ndani ya nyumba ambapo vyombo vya usalama walishindwa kuingia ndani ili kuthibitisha kama yupo huyo mtoto hii ni kutokana na kuwepo moto mkali ndani ya nyumba hiyo.
Waliobahatika kutoroka kwenye mkasa huo ni Adriani Henerico na familia yake ambaye alikuwa mwalimu katika shule ya msingi Mugaba lakini mali pamoja na nyumba yake ziliharibiwa mashamba kufyekwa na kuchomwa moto.
Mwingine aliyesalia katika familia ya Henerico John ni Froliani Henerico miaka( 46) ambaye aliachwa na watu waliotenda tukio hilo kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa ametengwa na familia hiyo kipindi cha miaka 10 kutokana na kutokubaliana na vitendo walivyokuwa wanavitenda ndugu zake.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii katika eneo la tukio Frolian Henerico aliyebahatika kuachwa salama na mali zake alisema kuwa wananchi wa kijiji hicho na maeneo jirani walikuwa wamechoshwa na vitendo vya ushirikina na ujambazi walivyokuwa wanafanya wanafamilia hao na yeye kuachwa walikuwa wakijua alivyotengwa na ndugu kwasababu ya kutokubaliana nao.
“Ndugu mwandishi wa habari nimetengwa na familia yangu kwa kipindi cha miaka kumi nimejaribu kwenda kwenye baraza la kata kusuluhisana lakini ilishindikana na niliambiwa tukae tuyamalize ndiyo maana nilikubali kutengwa na ndugu zangu”Alisema Frolian
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mugaba Justinian Clemence alisema kuwa yeye alifuatwa nyumbani na wananchi na ndugu za mfanyabishara aliyeuwawa wakiwa na mwenyekiti wa Kitongoji cha Omukicherenje wakitaka kuanza msako wa kumtafuta ndugu yao baada ya kuwa haonikani na aliaga kuwa anafuata mzigo wake kwa Datusi Paulo ndipo aliwakubalia na kuenda nyumbani kwa mtuhumiwa huyo.
Alisema kuwa baada ya kufika nyumbani kwa mtuhumiwa wakiwa kwenye mahojiano mafupi waliona damu na kuanza kufuatilia ilikoelekea ndipo waliona sehemu ikiwa imechimbuliwa na walipofukua waliona mwili wa mtu ndipo hasira za wananchi zilianzia hapo.
Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Luten Edward … akiongea na wananchi katika eneo la tukio na kujionea hali halisi na baadae kuongea nao huku akiwataka kutojichukulia sheria mkononi kwani kufanya hivyo vyombo vya usalama vitakosa taarifa muhimu za kiuchunguzi na kuongeza kuwa wanapopata taarifa za kiuharifu na uvunjifu wa amani watoe taarifa kwa vyombo vya dola ili viweze kuchukua jukumu lake la kufanya uchunguzi na hatimaye sheria ichukue mkondo wake.
“Ni kweli tukio hili linaweza kukupandisha hasira kwani kumuua mtu na kumfukia kwenye shimo si jambo rahisi lakini nyinyi wananchi msiwe wepesi wa kujichukulia sheria mkononi ona sasa aliyeua ameuwawa na ndugu zake wengine mali na zenyewe mmeteketeza tulizoea kusikia kwa wenzetu wakulya, wamasai lakini nyinyi akinamshomile tunajua ni wastaarabu lakini mmeanza kutisha kiasi hiki?”Alihoji Luten Mstaafu Edward
Mkuu wa wilaya alihaidi kukaa pamoja na wananchi wa kijiji hicho kwa ajili ya kuongea nao kwa kina ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo ili amani na utulivu ulirejee kwenye eneo hilo na wananchi waweze kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.
Hata hivyo hadi mwandishi wa habari hii anatoka kwenye eneo la tukio aliacha jeshi la polisi wakiendelea na taratibu za kiuchunguzi na kusema kuwa watatoa taarifa rasmi na mwili wa mfanyabiashara aliyeuwawa ulifukuliwa na kufanyiwa uchunguzi na daktari kisha kuupeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya Nyakahanga wilayani Karagwe,huku miili ya waliochomwa moto kukabidhiwa kwa uongozi wa serikali ya kijiji cha Mugaba kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi katika wilaya ya Karagwe na Kyerwa kwa mwezi wa saba vinazidi kuongezeka kila siku ambapo Julai 8 mwaka watu wanne(4) waliuwawa katika kijiji cha Kanogo kata ya Nyakabanga Julai 14 mwaka huu watu wanne(4)waliuwawa katika eneo la masheshe kata ya Nyakasimbi wote waliouwawa walituhumiwa kujiuhisha na vitendo vya uharifu kwenye jamii.

No comments:
Post a Comment