Jeshi la polisi wilayani Missenyi
Mkoani Kagera linamshikilia mtu mmoja
kwa kosa la kumpiga na kumuua mke wake.
Tukio hilo limetokea usiku
wa kuamkia Januari11 mwaka huu ,ambapo mwanaume aliyefahamika kwa jina la Kamala Kamugisha wa umri miaka 33 mkazi wa kitongoji Bwoba kijiji cha Kashaba wilayani
Missenyi amemuua mkewe kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake.
Akizungumzia tukio hilo Baba
Mkwe wa maraehemu Mzee Karoli
Kamugisha amesema kuwa kijana
wake ambaye ni mtuhumiwa sasa,amekuwa na ugomvi wa siku nyingi na mkewe hali
ambayo imepelekea hadi kifo hicho.
Mzee Karoli amesema kuwa
marehemu Laulensia Kamala usiku
alikimbilia kwa baba mkwe akidai kupigwa
na mmewe,ambapo alfajiri amekata roho wakiwa kwenye harakati za kumkimbiza
hospitalini.
Afisa mtendaji Abdalah Lutaiwa wa kijiji Kashaba amesema kuwa
marehemu ameuwawa kwa kupigwa mateke na ngumi sehemu mbalimbali za mwili
wake,huku akiwaasa wanaume ambao ni vijana kuacha tabia ya kujichukulia sheria
mikononi kwa kuwadhuru wake zao.
Amesema ili kukomesha
vitendo hivyo watahakikisha wanawachukulia hatua kali za kisheria wanaume ambao
watakuwa wanajihusisha na vitendo vya kuwanyanyasa wanawake katika familia.
Hata hivyo jeshi la
polisi wilayani humo limeruhusu mwili wa
marehemu kuzikwa na mtuhumiwa
anashikiliwa kwa ajili ya hatua zaidi za
uchunguzi.
No comments:
Post a Comment