Familia ya aliyekuwa Rais wa tano wa Zanzibar DK Salmin Amour imetapeliwa katika kijiji cha Magamba kata ya Kwaluguru wilayani Handeni mkoani Tanga kwa kuuziwa ekari 150 za ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo na baadae kubainika kuwa eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya hifadhi ya kijiji hicho.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Magamba Erick Semsela alikiri kupokea kiasi cha shilingi millioni mbili kwa ajili ya kuuza eneo hilo la hekari 50 tu na siyo eneo lote la hekari 150 kama inavyodaiwa huku akibainisha kuwa eneo la hifadhi ni hekari 15 tu.
Diwani wa Kata ya Kwaluguru Salimu Muya ameunda kamati itakayochunguza migogoro ya ardhi katani humo na kuipa siku 14 na baadae watoe majibu ya uchunguzi huo na kusema kuwa fedha na stakabadhi za hekari 100 hazionekani mahali ziliporekodiwa wakati mnunuzi anadai alilipa pesa yote na adaiwi.
Mwakilishi wa familia ya Rais Mstaafu Munil Amour amesema mwaka 2015 walifika kijijini hapo wakitafuta eneo la kufanyia shughuli za kilimo na kupatiwa eneo hilo na kufanya malipo lakini baadae ndipo ikabainika kuwa ni eneo la hifadhi na hawajui lini watapatiwa majibu ya ufumbuzi wa tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment