Watu sita wamefariki dunia na 25 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizotokea eneo la Iyovi katika daraja mto Ruaha na Dumila mkoani Morogoro
Kamanda wa polisi mkoa wa MOROGORO Leonald Paulo amesema tukio la kwanza lilitokea eneo la Msosa mpakani mwa Morogoro na Iringa katika daraja la Mto Ruaha katika mto mdogo wa Mkosi ambapo watu watatu walifariki dunia na wengine 20 kujeruhiwa vibaya.
Katika ajali ya pili iliyotokea leo Januari 02 mwaka huu 2016 majira ya asubuhi eneo la Dumila watu watatu wamefariki dunia papo hapo baada ya gari ndogo aina ya Toyota Vista kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa na tela lake na kwenye ajali hiyo watu watano wamejeruhiwa.
No comments:
Post a Comment