Watu wanne wa familia moja
katika kijiji cha Nyakahita kata ya kanoni wilayani karagwe wamenusurika kufa
baada kutegewa sumu kwenye chakula usiku wa kuamkia leo januari 11 mwaka huu.
Familia hiyo yenye jumla ya
watu wa nane wamewekewa sumu katika chakula na
wengine wanne walinusurika kura chakula hicho baada ya kuwaona wenzao
walioanza kura chakula hicho wakisumbuliwa na tumbo.
Akizungumzia juu ya tukio
hilo Mwenyekiti wa kijiji hicho ambaye pia ni shuhuda ya tukio hilo CHRISTOPHER
JUSTINIAN ameeleza kuwa baada ya tukio hilo walitakiwa kuitisha kikao cha dhalura
cha kijiji na kuwataka wananchi kutochukua maamuzi magumu yanayo gharimu maisha
ya watu wengine katika jamii wanapokwazwa na ndugu, jamaa na rafiki.
Aidha mwenyekiti huyo
ameongeza kuwa watu wanatakiwa kumjua mungu kwa kufanya maombi ili kuepusha
matatizo yanayo endelea kutokea katika jamii na endapo mwenzako akakukosea ni
vyema ukampeleka katika vyombo vya sheria kuliko kujichukuria sheria mkononi.
No comments:
Post a Comment