Monday, January 11, 2016

HABARI MPASUKO AVULIWA UKUU WA SHULE YA SEKONDARI KWA KUWATOZA WAZAZI MICHANGO YA MLINZI NA UJI





Katibu  Tawala  wa Mkoa  wa  Kagera  Nassoro  Mnambira  amemvua  madaraka  Mkuu  wa  Shule  ya  Sekondari  Bilele  iliyoko  Manispaa  ya  Bukoba  Siasa  Phocus  kwa  kukiuka  maelekezo  ya  serikali  kwa  kuwataka  wazazi  na  walezi wa  wanafunzi  kutoa  fedha ya  michango  ikiwemo  shilingi  elfu  arobaini  za  uji  na  fedha  za  mlinzi  shilingi  elfu  tano.

Amesema  kitendo cha  mkuu  huyo  kutoza  michango  hiyo  ni  kukiuka  agizo  la  Rais   aliyesema  elimu  ni  bure  huku  akitoa  ufafanuzi  juu  ya  mkoa  wa  Kagera  kupokea  fedha  kutoka  hazina  kwa  ajili  ya  kutekeleza  tamko  la  elimu bure.

Kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi mkoa wa KAGERA umepokea shilingi milioni 810 laki moja na 57 elfu kwa awamu ya kwanza  ili kutekereza sera ya elimu bure.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu tawala wa mkoa wa KAGERA NASORO MNAMBIRA amesema kuwa milioni 309 laki nne 61 elfu zimepelekwa katika shule za msingi huku zaidi ya milioni mia tano zikipelekwa katika shule za sekondari mkoani KAGERA.


Akitoa  ufafanuzi wa fedha hizo zilivyopokelewa katika halmashauri za mkoa wa KAGERA amesema kuwa kwa upande wa shule za sekondari  wilaya ya Bihalamuro imepokea milioni 76,halmashauri ya Bukoba ya milioni 36 Bukoba manispaa milioni 122 Karagwe milioni 36 Kyerwa milioni 21 Missenyi milioni 29 muleba shilingi  milioni 93 na Ngara shilingi  milioni 60.


Kwa upande wa fedha zilizopokelewa katika shule za msingi  kwa mkoa wa KAGERA wilaya ya Buhalamuro imepokea shilingi milioni 43,halmashauri ya Bukoba zaidi ya milioni 36, bukoba manispaa zaidi ya milioni 27 karagwe zaidi ya milioni 37 kyerwa zaidi ya milioni 37 misenyi zaidi milioni 20 Muleba milioni 69 na Ngara milioni 37.

No comments:

Post a Comment