Kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge ya uchaguzi mkuu 2015 jimbo la Kyerwa Mkoani Kagera inatarajiwa
kuanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza Alhamisi ya tarehe 21 januari mwaka huu.
Akiongea na MTANDAO HUU aliyekuwa mgombea wa ubunge
katika jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, Benedicto
Mtungirehi amesema baada ya kufuata taratibu za mahakama zilizokuwa
zinahitajika sasa kesi hiyo inategemewa kusikilizwa kwa mara ya kwanza.
Mtungirehi amesema amekuwa akipokea maswali mengi kutoka
kwa wananchi wa Jimbo la Kyerwa kuhusu
kesi iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba ambapo amesema kuwa
ilikuwa vigumu kuwajibu kwani kesi ilikuwa bado haijaanza kusikilizwa lakini sasa kesi hiyo
itasikilizwa kwa mara ya kwanza januari 21 mwaka huu.
Ameeleza kuwa siku ya Alhamis mshitaki na mshtakiwa wanatakiwa
kufika katika mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba kwa ajili ya kupanga
mambo ya msingi ya namna ya kuendesha kesi hiyo.
No comments:
Post a Comment