Mkuu wa mkoa wa Kagera John
Mongella amewataka wazazi,walezi na
Jamii kwa ujumla kuwapeleka watoto wote wanaotakiwa kujiunga na elimu ya msingi
pamoja na sekondari mapema iwezekanavyo kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Ameyasema hayo mapema
leo katika ziara yake ya kukagua usajili
wa wanafunzi unavyoendelea katika wilaya
ya Karagwe.
Hata hivyo ametembelea mradi
wa ujenzi wa chuo cha ualimu uliopo Kata ya Ihanda wilayani hapa na kuhaidi kutoa
ushilikiano juu kumalizia mradi huo.
Aidha ametoa
agizo kwa uongozi
wa wilaya ya
Karagwe kuhakikisha ifikapo Machi
Mosi mwaka huu
watoto wote wawe wameisharipoti madarasani
kwani ni lengo la mkoa mzima
wa Kagera kwa
tarehe hiyo.
No comments:
Post a Comment