Monday, January 4, 2016

WAKAZI WA KINONDONI WA BOMOABOMOA WATINGA MAHAKAMANI WAAMBIWA WAVUTE SUBIRI MPAKA KESHO.






Hatima ya  maombi  ya  wakazi  wa  jimbo  la  Kinondoni ambao  nyumba  zao  ziko  katika  orodha  ya  bomoabomoa itajulikana  kesho  mahakama  ya  kuu  kitengo  cha  Ardhi  itakapotoa  uamuzi wa  maombi  yao  ya  kusimamisha  uamuzi wa  serikali  kuwabomolea ili  kusubiri usikilizwaji wa  maombi  yao  ya  kibali cha  kufungua  kesi  kupinga   ubomoaji  huo.




Wakili wa wakazi  wa  Kinondoni ,Abubakar   Salum aliiomba  Mahakama itoe  amri kwamba  hali iendelee kuwa  kama  ilivyo kwa  sasa  kusubiri  usikilizwaji  na  uamuzi wa  maombi  ya  kibali  cha  kufungua  kesi lakini  wakili  wa  serikali  Gabriel  Malata alipinga  ombi  hilo akidai kuwa  waombaji hao  hawana  haki ya  kuomba  amri  yoyote ya  mahakama   katika  hatua  hiyo  ambapo  Mahakama  haijawapa  kibali  cha  kufungua  kesi.



Jaji  Panterine  Kente  baada  ya kusikiliza hoja  za pande zote alisema  kuwa  atatoa  uamuzi  wake  kesho saa  tano iwapo hali ilivyo kwa  sasa iendelee au  la.

No comments:

Post a Comment