Tuesday, March 27, 2012

HII NDO UTAWALA WA NCHI YETU

Serikali ya mtaa wilayani Karagwe yavamia wananchi kudai michango usiku wa manane.

.
Karagwe-Kagera.

                                        Mwananchi aliyejeruhiwa na wanamgambo waliokodiwa kutoka kata jirani ya    
                                        Mabira wilayani Karagwe (Dereva aliyewapakia wanamgambo).

KUFUATIA  ujenzi wa shule za sekondari unaoendelea nchini kote, wananchi wa kata ya Kanoni wilayani hapa wamelalamikia kile kinachodaiwa ni uvamizi dhidi yao unaofanywa na viongozi wa serikali ya mtaa wao kudai michango usiku wa manane. Wananchi wa kata hiyo walivamiwa na wanamgambo walikodiwa kutoka kata ya Mabira Usiku wa kuamkia machi 16 mwaka huu ambapo wanamgambo wanadaiwa kukodi gari usiku wakidai linaenda kupakia saruji na kwenda kuvamia wananchi wa kitongoji cha Katabwoba kata ya Kanoni kwa madai kuwa wanahitaji michango ya ujenzi wa sekondari. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Karagwe Bw.Gregori Gabone akiambatana na Katibu wake Bw. Geofre Nguma walifika eneo la tukio na kubaini kuwa wananchi hao wanazo stakabadhi zinazothibitisha kuwa wananchi hao walishalipa michango muda mrefu. Wameulaumu uongozi wa serikali ya mtaa huo kwa kuwanyanyasa wananchi bila sababu. Kwa mujibu wa Bw Gabone, Mwenyekiti wa Kata ya Kanoni  Bw. Patrick Byarushengo anadaiwa kuongoza uvamizi huo ambapo wamevunja nyumba ya mzee Severin Mathayo (56) mkazi wa kitongoji hicho, Prosper Innocent, na Bi Eufrasia (46)  ambao wote walipelekwa hospitali ya Nyakahanga na kubainika kuumizwa vibaya na kipigo walichopewa na wanamgambo hao.Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Karagwe Bi Adventina Kahatano amesema kuwa kinachopelekea hali hiyo ni kukiuka taratibu za utozaji wa michango akimaanisha kuwa wananchi hawajashirikishwa kikamilifu. Amedai kuwa wananchi wanapaswa kushirikishwa na wabaini vipaumbele vyao.
Diwani wa kata ya Kanoni Bw. Sabby Rwazo alipoulizwa kuhusiana na utaratibu huo wa kudai michango usiku wa manane alidai kuwa haikuwa usiku kwani alipigiwa simu juu ya tukio hilo saa 11 alfajiri tarehe 16 mwezi Machi. Hadi Machi 22 diwani huyo hakusema juu ya tukio hilo ambapo siku hiyo Radio Karagwe ilimtafuta bila mafanikio.
Katika tukio hilo ilipigwa yowe iliyopelekea wananchi kujitokeza na kuanza kutembeza kipigo wakianza nadereva ambaye pia alipoteza pesa Tsh 50,000/=


Nyumba ya Bwana Severin Mathayo iliyovamiwa.


No comments:

Post a Comment