Maandalizi ya kuadhimisha miaka miamoja tangu kuanzishwa kwa hospitali ya Nyakahanga yanaendelea kushika kasi, baada ya kamati ya uhamasishaji kuteua kauli mbiu ya maadhimisho hayo ijulikanayo kama 'Shabaha yetu ni huduma bora za afya na tiba '
Kikao cha kupitisha kaulimbiu hiyo kilichofanyika hivi karibuni chini ya mwenyekiti wake Dr. Butoto, kiliamua kaulimbiu hiyo itumike baada ya kubarikiwa na mwenyekiti wa kamati kuu ya maandalizi ya jubilee hiyo Dr. Andrew Cesari ambayo tayari imeanza kutumika rasmi
HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA
KARAGWE NYAKAHANGA
Katika kujali jamaii ya wana Karagwe, uongozi wa KKKT Dayosisi ya Karagwe umeona ni bora kuanza uhamasishaji kwa kutumia vyombo vya habari vilivyomo katika wilaya hiyo kimojawapo ni Radio Karagwe kupitia masafa yake ya 91.4 FM.
Hosptali teule ya wilaya ya Karagwe Nyakahanga ilianzishwa miaka miamoja iliyopita ambapo juma la maadhimisho ya jubilee yake yatafanyika kuanzia Agost 27 na kilele chake ni septemba 2 mwaka huu.
"HUDUMA BORA ZA FYA NA TIBA"
Maadhimisho hayo yatakwenda sambamba na harambee ya ujenzi wa chuo cha wataalam wa afya na tiba kitakacho jengwa wilayani Karagwe.
Karagwe-Kagera
WAKATI hospitali ya Nyakahanga ikijiandaa kuadhimisha miaka 100, Zaidi ya shilingi bilioni moja nukta nane zinahitajika kufanikisha ujenzi wa chuo cha uuguzi wilayani Karagwe mkoa wa Kagera kitakacho kuwa chini ya Kanisa la Kiinjili la Kiluuther Tanzania dayosisi ya Karagwe.
Kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo inajipanga kufanya harambee itakayoiwezesha ELCT Karagwe kupata fedha za ujenzi wa chuo hicho amabcho kinatarajia kuchukua wanafunzi wa mwaka wa kwanza mwakani.
Ujenzi wa chuo hicho unatarajia kwenda sambamba na maadhimisho ya jubilee ya miaka miamoja ya tangu kujengwa kwa hospitali ya Nyakahanga iliyoko chini ya ELCT iliyoanza kutumika tangu mwaka 1912
Ujenzi wa chuo hicho huenda ukapunguza tatizo la wauguzi katika hospitali ya Nyakaganga na kwengineko wilayani hapa.

Wapo wataalamu wengi waliopita katika hospitali yaNyakahanga Karagwe kiutumishi na hata kimatibabu je unaonaje kujitokeza kuchangia ujenzi wa chuo hicho? "kamati ya uhamasishaji"
Ni muda mfupi namba za mawasiliano na mfuko wa uchangiaji vitatangazwa na kupitia blog hii unahamasishwa kujitokeza kuchangia mala tu njia hizo zikitangazwa.
ASKOF BENSON BAGONZA
DAYOSISI YA KARAGWE-KAGERA
Hospitali ya Nyakahanga kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa.
Wakati hospitali ya nyakahanga ikijiandaa kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa mwaka 1912, sasa zaidi ya sh bilioni moja zinahitajika kufanikisha ujenzi wa chuo cha uuguzi karagwe mkoani Kagera
Hospitali hiyo iliyopo chini ya kanisa la ELCT Dayosisi ya Karagwe, inakabiliwa na tatizo kubwa la uhaba wa wauguzi na Huenda ujenzi wa chuo hicho ukikamilika utapunguza tatizo hilo wilayani humo na mkoa mzima kama siyo tanzania nzima
ASKOFU BENSON BAGONZA
WA DAYOSISI YA KARAGWE
kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya jubilee hiyo Dr Endrew ambaye pia ni mganga mkuu wa hospitali hiyo, tatizo la uhaba wa wauguzi katika hospitali hiyo ni kutokana na wauguzi wengi kutoka nje ya mkoa jambo linalowapa shida ni jinsi ya kuzoea hali ya mazingira

No comments:
Post a Comment