Saturday, March 24, 2012

MATOKEO YA LIGI YA ENGLAND

Saturday, March 24, 2012


Matokeo Ligi Kuu ya England leo

LONDON, EnglandARSENAL imeendelea kufanya kweli katika Ligi Kuu ya England baada ya kuibandua Aston Villa mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa kwenye Uwanja wa Emirates.
Arsenal wakishangilia
Mabao ya Kieran Gibbs, Theo Walcott na Mikel Arteta yanaifanya Arsenal kufikisha pointi 58 mbele ya Man United na Man City zinazoongoza ligi hiyo. Man United ambayo kesho inacheza na Fulham ina pointi 70 wakati City iliyokuwa ugenini jana usiku ilikuwa inacheza na Stoke City.
Ushindi na uhakika wa kuendelea kushikilia nafasi ya tatu ulichangiwa pia na suluhu ya Chelsea dhidi ya Tottenham ambazo ziko nafasi ya nne na tano. Chelsea sasa ina pointi 50 wakati Totts wamefikisha pointi 55.
Nayo Liverpool ikiwa kwenye uwanja wake wa Anfield, imeendelea kuwa nyanya baada ya kutandikwa mabao 2-1 na Wigan katika mechi iliyokuwa ya ushindani.
 Shaun Maloney alikuwa wa kwanza kufunga kabla ya Luis Suarez kusawazisha dakika ya 46. Gary Caldwell alimaliza nguvu za Liverpool kwa kuandika bao la pili.
Bolton ilipata faraja ya kumkosa Fabrice Muamba kwa kuilaza 2-1 Blackburn sawa na Norwich ilivyoitungua Wolves huku Sunderland ikiizabua 3-1 QPR. Swansea iliyokuwa nyumbani ilifungwa mabao 2-0 na Everton.

No comments:

Post a Comment