Wednesday, April 18, 2012

HII NILIJARIBU KUPATA TAKWIMU MAENEO MENGINE NILIFIKA MWENYEWE

Takwimu Na hali ya  Ukimwi  Tanzania  

Siku  ya Ukimwi dunian ilianzishwa maalumu  kuadhimishwa siku ya tarehe 1.12. kila mwaka kwa kuwa siku ya kwanza  kugundua   kirus kinachoeneza   ugonjwa  wa Ukimwi kiligunduliwa siku ya tarehe 1.12 .mwaka  1981
Mwaka 1983  ndo mgonjwa wa kwanza  wa Ukimwi aligunduliwa katika hospitali ya Ndolage  iliyopo  mkoani Kagera  mgonjwa huyo alitokea kijiji cha Kanyigo Bukoba vijijini sasa wilaya ya Missenyi.

Tangu kugunduliwa  kwa ugonjwa wa Ukimwi  nchini mwetu watu wapatao  1.3 milion wanaishi na virusi vinavyoeneza ugonjwa  wa Ukimwi  na kati ya hao watu wapatao  384,816    tayari wameanzishiwa  dozi ya dawa ya kupumbaza virus  vya Ukimwi yaani  ARV’S  na  watu wapatao 86,000 wamepoteza  maisha kutokana  na ugonjwa  wa ukimwi  na kuacha watoto yatima 2 milion   kutokana na kufiwa  na wazazi wao na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.Kuanzia  Julai  2007 watu 13 milion wapima afya zao kwa hiari na Ushauri Nasaha pale rais wa  JAKAYA KIKWETE alipozindua  kampein ya upimaji  wa hiari  imesaidia kupunguza unyanyapaa.

Kufikia  Desembar  2010  watu wapatao 740,040  wanaoishi  na virus vya Ukimwi  walipata huduma  ya matibabu na uangalizi,na kati ya hao 384,816 wako katika dozi ya ARV’S  hii ni sawa na 87.5 ya walengwa kupata matibabu.Kwa sasa  kuna vituo 4,301 vya kutoa huduma ya kinga ya maambukizi ya mama  kwenda  mtoto(PMTCT) Ikiwa ni sawa na 93% kwa vituo vya afya vilivyolengwa.Kufikia mwaka 2010 wanawake wajawazito waliokuwa wakiishi na HIV  ni 80,748 sawa na 70% na kati ya hao 65,948 waliopata matibabu sawa na 57% na walipokea madawa ya kukinga maambukizi  ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
 
 Kwa  Takwimu  zilizotolewa  na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania  TACAIDS kuhusu  hali ya maambukizi  Tanzania Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa   mwaka  2007-2008 kiwango cha maambukizi kitaifa  kilishuka kutoka asilimia 7.7 ya mwaka 2003-2004 mpaka 5.1  huku mikoa 5 inayoongoza kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2007/2008 ikiwa ni  Iringa 15.1%,Dar-es salaam 9.3%, Mbeya  9.2%,Mara 7.7%  na Shinyanga 7.4% huku mkoa unaoongoza kwa maambukizi mpya hivi sasa  ni Mara ambao umeongeza 3.5%  kutoka 4.2% za mwaka 2003/2004 nakufikia 7.7% za mwaka 200/2008.
Wilaya zinazoongoza  kwa maambukizi  kitaifa  kwa sasa  ni Makete ya mkoa wa Iringa ,Rory kwa Mkoa wa Mara .
 
Mitandao
Print
 
Kwa Ujumla neno mtando lina maana ya mfumo au kikundi chochote kilichounganishwa. Hii ni njia mojawapo ya kubadilishana habari kati ya mifumo tofauti. TACAIDS inaratibu mitandao mbalimbali ya mapambano dhidi ya UKIMWI. Ifuatayo ni baadhi ya miandao hiyo:
  1. NETWO+: Ni Mtandao wa Taifa wa Wanawake wenye VVU/UKIMWI
  2. ICW: Ni Jumuiya ya Kimataifa ya Wanawake wanaoishi na VVU/UKIMWI
  3. MNEYOP+ : Ni Mtandao wa Taifa wa Vijana wenye VVU/UKIMWI
  4. TANGYWA+:Ni Mtandao wa Taifa wa Wasichana na Wanawake Vijana wanaoishi na VVU/UKIMWI Tanzania
  5. TANEPHA:Ni mtandao wa Asasi za Watu wanaoishi na VVU/UKIMWI Tanzania
  6. TANERELA :Mtandao wa Viongozi wa Dini wanaoishi au walioathiriwa na VVU/UKIMWI Tanzania
  7. NYP+ :Mtandao wa Vijana wanaoishi na VVU/UKIMWI
  8. NACONGO :Baraza la Taifa la Asasi zisizo za Serikali
  9. TAYOPA :Balozi wa Vijana wanaoishi na VVU/UKIMWI Tanzaniaa
  10. FONEPHAT :Mtandao wa Kitaifa wa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI
  11. NACOPHA:Baraza la Taifa la watu wanaoishi na VVU/UKIMWI Tanzania

NACOPHA: Ni Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU/UKIMWI Tanzania ni asasi isiyo ya serikali iliyoanzishwa mwaka 2003 kwa madhumuni yaliyotajwa katika kifungu cha 2.4 cha katiba yao kama ifuatavyo: Kuwakutanisha watu wanaoishi na VVU/UKIMWI kwa madhumuni ya kuongeza ushiriki na kuongeza uwezo wao wa kushawishi katika majukumu yao katika kufanikisha mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI nchini Tanzania. NACOPHA ilianzishwa kama asasi mwavuli kwa mujibu wa dira na dhamira iliyotajwa katika katiba yao.

FONEPHAT: Ni Mtandao wa Kitaifa wa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI. Ni asasi mwavuli kwa ajili ya mitandao, vikundi na vyama vya watu wanaoishi na VVU/UKIMWI nchini. Ina jukumu la kuratibu mitandao ya WAVIU Tanzania. FONEPHAT ilianzishwa mwaka 20 Oktoba, 2007 mjini Dar es Salaam ambapo kwa sasa inaratibu mitandao 12 ya kitaifa ya WAVIU. FONEPHAT ina bodi na sekretariati.

TAYOPA: Ni Balozi wa Vijana wanaoishi na VVU/UKIMWI Tanzania. Ilianzishwa mwaka 1998 na kusajiliwa rasmi mwaka 2001. Inaongozwa na Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina. Vile vile ina kamati ya utendaji, maamuzi makuu hufanywa na mkutano mkuu ambao hukutana kila baada ya miaka mitano (5). TAYOPA ina matawi 4 katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Ruvuma na Rukwa. Jukumu kubwa la TAYOPA ni kuelimisha vijana walioko mashuleni na wasio kuwa mashuleni.

NACONGO: Ni chombo chenye jukumu la kuratibu na kujiratibu kwa asasi zisizo za serikali zinazofanya kazi Tanzania. NACONGO ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 24 ya mwaka  2002, na kuzinduliwa rasmi mwaka 2003.

ICW: Ni Jumuiya ya Kimataifa ya Wanawake wanaoishi na VVU/UKIMWI. Ni mtandao wa kimataifa pekee unaoendeshwa kwa ajili ya na wanawake wenye VVU/UKIMWI. Ilianzishwa mwaka 1992 na wanawake 56 wenye VVU/UKIMWI duniani. Uanachama wa ICW ni huru na unawahusu wanawake wenye VVU/UKIMWI tu. ICU inahusu masuala na mahitaji yanayowakabili wanawake wanaoishi na VVU/UKIWM duniani kote na kuunda msingi wa philosophia ya asasi hiyo. Wanawake walikubaliana wasikate tama na ndio maana walianzisha jumuiya hiyo. ICW inajihusisha zaidi na uraghbishi kuhusu masuala ya wanawake.

NETWO+: Ni mtandao wa Taifa wa Wanawake wenye VVU/UKIMWI. Mtandao huu unafanya shughuli zake nchi nzima na unaendeshwa na wanawake wanaoishi na  VVU/UKIMWI. Ulianzishwa mkoa wa Morogoro Decemba 28, 2002 na kusajiliwa rasmi Mei 30, 2003 kwa namba ya usajili SO11944. Ilianzishwa kwa madhumuni ya kuunganisha wanawake wanaoishi na VVU/UKIMWI na watu binafsi, vikundi na asasi zinazosaidia wanawake wenye mahitaji yanayohusiana na VVU/UKIMWI.
Lengo kuu la mtando huu ni kuongeza fursa ya wanawake wanaoishi na VVU/UKIMWI za kusikika na kushiriki katika shughuli za kidemokrasia zinazowezesha kusikika kwa haki zao na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wadau na wahisani wengine.
TANERELA
TANERELA ni Mtandao wa Viongozi wa Dini Waishio na VVU au Walioathiriwa Binafsi na VVU/UKIMWI. Mtandao huu ulianzishwa kwa nia ya kuwawezesha viongozi wa Dini wanaoishi na VVU na wale walioathiriwa binafsi kufanya yafuatayo:
  • Kuvunja ukimya na kuwa wazi kuhusu hali zao;
  • kuondoa unyanyapaa binafsi – Kujinyanyapaa
  • kuondoa mtazamo hasi wa kukana na kukataa ukweli wa hali halisi
  • Kuondoa mawazo ya kudhani kwamba kuwa na VVU ni jambo la aibu
  • kuwa chachu ya mabadiliko kiimani kwa wao wenyewe, kwa Jamii zinazowazunguka na kwa Taifa kwa jumla
  • Makao Makuu ya TANERELA yako Dar es Salaam lakini pia ina matawi katika mikoa ya Dodoma, Kagera, Kigoma na Morogoro.

TANOPHA
TANOPHA ni mtandao wa Asasi za Watu Waishio na VVU/UKIMWI ambao ulianzishwa mwaka 2001 na kusajiliwa 2002. TANOPHA ilianza na asasi wanachama 22 na kwa sasa ina jumla ya wanachama 110 kwa nchi nzima.
TANOPHA Ilianzishwa kwa lengo la kuzipa nguvu na sauti na kuzisaidia asasi zinazoendeshwa na kungozwa na watu waishio na VVU katika Tanzania. Makao makuu ya TANOPHA yako Dar es Salaam

TANEPHA
TANEPHA ni mtandao wa watu waishio na VVU uliosajiliwa mwaka 2003 kwa lengo la kushirikiana na mitandao mingine ya ndani na nje ya nchi ili kuunganisha juhudi katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kuwa kituo cha Taarifa za kimataifa kwa WAVIU. Aidha TANEPHA inahusika pia na kufuatilia suala la upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya VVU kwa walengwa.
 
TANGYWA+
TANGYWA+ ni mtandao wa wasichana na Wanawake vijana wanaoishi na VVU ulioanzishwa mwaka 2004 na kusajiliwa mwaka 2007. Mtandao huu unalenga kudhibiti maambukizo mapya ya VVU, kupigania haki za binadamu, afya ya uzazi kwa wasichana na wanawake wa umri Mdogo.
Miongoni mwa shughuli za TANGYWA+ ni kuboresha hali za maisha ya wasichana kwa kutoa huduma zifuatazo:
  • Misaada wa kimaadili, na kisaikolojia kwa wateja wake;
  • Misaada ya lishe na vifaa vya shule kwa watoto yatima;
  • kutoa maelekezo na ushauri kuhusu masuala ya tiba na matunzo kwa wagonjwa wa UKIMWI;
  • Huduma za tiba, ushauri na matunzo nyumbani;
  • mafunzo ya stadi za maisha kwa wasichana
  • Hivi sasa mtandao huu unafanya kazi katika mikoa 8 ifuatayo katika Tanzania Bara: Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kilimanjaro,Morogoro, Mwanza, Singida na Pwani.

NNEYOP+

NNEYOP ni mtandao wa kitaifa wa Vijana Wanaoishi na VVU ulioanzishwa na kusajiliwa mwaka 2006 kwa ajili ya kuchangia juhudi za serikali za kudhibiti maambukizo ya VVU na UKIMWI nchini Tanzania.
Lengo la NNEYOP+ ni Kuunganisha vijana wanaoishi na VVU waweze kupigania haki zao na kutetea haki za vijana wanaoishi na VVU yakiwemo masuala ya unyanyapaa na ubaguzi. Aidha NNEYOP inatetea uimarishaji wa huduma za tiba, matunzo na misaada kwa vijana waishio na VVU na ushirikishwaji wao kwenye vyombo vya maamuzi.
 
Prepared   by
Juhudi  felix
2012
 
No comments:

Post a Comment