Wednesday, April 18, 2012

HIVI KARIBUNI NITAWAWEKEA BAADHI YA PICHA ZA WATU WENYE ULEMAVU KTK UTAFITI TULIOFANYA PAMOJA NA WENZANGU CHINI YA UFADHILI WA MKURUGENZI WA REDIO FADECO FM.









RIPOTI    YA ZIARA YA KUTEMBELEA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KARAGWE.


1 UTANGULIZI:

Awali ya yote tunatanguliza shukrani za pekee kwa mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kufanya kazi hii wa kuwafikia walengwa ambao tuliokuwa tumewalenga na kutujalia uzima kuzitembea kilometa  haikuwa kazi rahisi kukamilisha kazi hii.

Tumejaliwa kuzitembelea kata zote 40 za wilaya ya Karagwe na Kyerwa na leo hii tupo hapa kuieleza jamii ya Karagwe na Tanzania kwa ujumla na sehemu nyingine ya jumuia za kimataifa kuwa Karagwe tunayo idadi kubwa ya watu wenye ulemavu mbalimbali kwa hiyo itambue ili atakayeguswa anaweza kuangalia ni kwa namna gani  anaweza kutoa mchango wake

Katika zoezi hili tumejaliwa kuongea na kuhoji watu wenye ulemavu wapatao watu 15575 wanaume wakiwa ni 879 na wanawake 676 hii ni idadi ya walemavu waliohudhuria siku ya ziara idadi itaongezeka pindi fomu tulizosambazwa zikirejeshwa tuna imani itaongezeka maradufu maana kutokana jiografia ya maeneo ya wilaya hii wengi hawakujitokeza pengine uhamasishaji hafifu wa viongozi na mwitikio wa jamii na walemavu wenyewe pia kama tulivyo ainisha katika ripoti hii.

Shukrani zetu pia tunazitoa kwa Mkurugenzi wa Redio Fadeco Joseph  Sekiku kwa moyo wake wa upendo na kusaidia ambao umeanzisha matumaini mapya kwa watu wenye ulemavu hapa wilayani Karagwe kuwapa fursa ya kupaza sauti zao ilikuwa ni faraja tosha kwani kupitia ziara hizi mwanga mpya umeonekana kwao maana kote tulikopita watu wenye ulemavu waliweza kuanza mara moja kuunda umoja wao kwa ajili ya kujadili masuala yanayowagusa na kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili wao wenyewe.

Baada ya shukrani hizo  tunaomba tuwape picha ya wilaya ya Karagwe ilivyo kwa wageni wapate kuifahamu wilaya hii  na   wilaya mpya  ya Kyerwa

 1.1 HALI YA WILAYA KWA UFUPI

Wilaya ya Karagwe ni kati ya Wilaya 8 za Mkoa wa Kagera .inapatikana katika Latitude nyuzi 1º hadi 20º Kusini ya Ikweta na Longitude 30º hadi 38º. 30” Mashariki mwa Greenwich . Wilaya inapakana na Nchi ya Uganda upande wa Kaskazini, Nchi ya Rwandaupande wa Magharibi, Wilaya ya Ngara upande wa Kusini na Wilaya ya Misenyi na Muleba upande wa Mashariki. Mto wa Kagera upo mpakani mwa Wilaya ya Karagwe na Nchi ya Rwanda na sehemu ya Kaskazini Magharibi mwa Nchi ya Uganda .

Wilaya ina eneo la Kilimita za Mraba 7,716,kati ya hizo Kilomita za Mraba 7,558 ni eneo la nchi kavu na Kilomita za Mraba 158 ni eneo la maji. Mwinuko wa Ardhi kutoka usawa wa Bahari ni Mita 1500 hadi Mita 1800. mwinuko mrefu ni Mlima wa Rwabunuka .Hali ya hewa kwa ujumla ni joto la wastani wa 20- 26ºC. Mvua zinanyesha kwa wastani wa Milimita 1,040 hadi 1,200 kwa Mwaka kati ya Mwezi September na Januari na kati ya Mwezi Machi na Mei.




1.2  UTAWALA
Kiutawala Wilaya imegawanyika katika Tarafa 9, Kata 40 Vijiji 166 na Vitongoji 1,373. Katika mgawanyiko huu, Tarafa 5 Kata 12 Vijiji 57 na Vitongoji 211 ni vipya. Tangu Mwezi Julai 2010 Serikali iliridhia ombi la kuanzisha Wilaya mpya ya Kyerwa, iliyo na Tarafa 4 Kata 18, Vijiji 93 na jumla ya Vitongoji 646. Tunayo majimbo 2 ya uchaguzi ya Karagwe na Kyerwa yaliyo na Wabunge wafuatao:-
- Jimbo la Karagwe- Mhe.Gosbert Blandes (CCM)
- Jimbo la Kyerwa- Mhe. Eustace.O.Katagira(CCM) Pia tuna jimbo la Kayanga  la  Kanisa Katoliki na Dayosisi ya Karagwe ya  Kanisa la Kiinjili la Lutheri  Tanzania(KKKT)

 1.3  IDADI YA WATU
Kwa mjibu wa Sensa ya Mwaka 2002 Wilaya ilikuwa na watu 423,423.
(Me 207,850 na Ke 215,573). Ongezeko la watu kwa Mwaka ni Asilimia 2.9. Hivyo inakadiliwa kwa kutumia ongezeko hilo Mwaka 2011 Wilaya ilikuwa na idadi ya watu wapatao 639,651.

1.4  HISTORIA YA WILAYA KWA UFUPI.

Wilaya ya Karagwe ilizinduliwa Mwaka 1958 na Gavana Richard Turnbull baada ya kumegwa kutoka katika Wilaya ya Bukoba. Kwa hali hiyo Wilaya ya Karagwe ilikuwepo wakati Tanganyika inapata Uhuru wake hapo tarehe 9/12/1961. Wakati huo shughuli za kiutawala zilikuwa zinafanyika katika maeneo mawili tofauti yaani Kayanga na Nyakahanga (yaani Ahalukiko). Baadae Kayanga ikawa ndiyo Makao Makuu ya kiutawala ambako Mkuu wa Wilaya alikuwa akifanya kazi wakati huo Nyakahanga palikuwa panatumiwa na Omkama kama Makao Makuu yake.

Baada ya kueleza hali ya wilaya kwa ufupi ninaomba niwarejeshe katika mada nzima au lengo mahususi kwa siku ya leo ambalo li,etujumuisha hapa kwa ajili ya kuona ni jinsi gain tunaweza kutatua changamoto na hali halisi ya watu wenye ulemavu katika wilaya hii ya Karagwe na wilaya mpya ya Kyerwa.

Kilichopelekea kuwepo zoezi hili la kuwatambua watu wenye ulemavu ni kuhamu hali halisi na kupata  yaliyokuwa wakielezwa mara kwa mara na Bwana Ashimu Muhamudu ambaye ni mwenyekiti wa watu wenye ulemavu hapa Karagwe akiwa akilalamika mara kwa mara kuwa watu wenye ulemavu wanakabiliwa na changamotonyingi ikiwemo jamii kuwanyanyapaa ,kutowashirikisha  kutowathamini  kuwa na wao wanastahili huduma stahili  sawa na watu wengine.

Kufuatia hilo Redio Fadeco chini ya Mkurugenzi wake aliona ni vema kujinyima kile kidogo ili waweze kwenda huko kwenye jamii kujua je hao watu wenye ulemavu ni kweli wapo na kama wapo ni kweli jamii inawanyanyapaana kutowathamini na kuangalia ni vipi viongozi wa ngazi husika wanawashirikishaje katika maamuzi ya masuala mazima ya shughuli za maendeleo  na mambo yanayowagusa wao moja kwa moja.Hali tuliyoibaini katika zoezi hili la utafiti wa kuwatambua ni pamoja na haya yafuatayo.

i)                    Jamii ya Karagwe na hata ya nje ya Karagwe ilikuwa haijui kabisa kuwa kuna idadi kubwa ya  watu wenye ulemavu hapa wilayani kwani kuna wengi waliokuwa wakihoji maswali wakitaka kufahamu kweli kuna  watu wenye ulemavu  katika wilaya hii.

ii)                  Hali ya kipato kwa familia ambayo mama au baba mmojawapo ni mlemavu ni duni na hali inayopelekea watoto wao kutoweza kumudu kumaliza shule nap engine kutoenda kabisa shule.
iii)                Viongozi wa ngazi ya kata vijiji na vitongoji kutowashirikisha kikamilifu katika shughuli za maendeleo na maamuzi ya mipango ya mambo yanayowagusa watu wenye ulemavu.
iv)                Kutokuwa na mtu wa kuwasemea katika vikao na wapi waelekeze sauti zao ili ziweze kusikia na kutatuliwa matatizo yao waliyonayo.
v)                  Kuna ulemavu mwingine unaweza kupatiwa ufumbuzi wa kimatibabu na kuondokana na tatizo hilo lakini  ni wapi waanzie na waelekee mfano ni ugonjwa wa Fistula na mdomo ulio wazi yaani mdomo wa sungura unatibiwa tatizo ni wapi wapate wa kuwaelekeza wanapotoa tiba
vi)                Kutokuwa na umoja wa watu wenye ulemavu ngazi ya kitongoji,kijiji na kata kitendo kinachowanyima fursa ya kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.
vii)              Viongozi na wanajamii  wa maeneo yote tuliyotembelea asilimia 85 hawatambui vema aina za ulemavu ni zipi mfano wao hujua kuwa mtindio wa ubongo si ulemavu,ugonjwa wa kifafa si ulemavu na aina nyingi za ulemavu  hali inayopelekea kuwepo unyanyapaaji.
viii)            Kuna idadi kubwa ya watoto wenye ulemavu kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu mfano walio na ulemavu wa kutoongea Bubu,tuliobahatika kuongea nae hawajui ni wapi watoto wao wanaweza kupata shule ili wakapate elimu  wapo tulio wapata Chanika,Nyakasimbi,Rutunguru na Rukuraijo mtoto Tumaini Silvester mwenye umri wa miaka 10 alirudishwa nyumbani toka shule ya Mgeza kwa kinachoelezwa kuwa ni kutokuwa na uwezo wa kujifulia mwenyewe nguo zao.
ix)                Kutokuwa na mitaji ya kuanzisha biashara ndogondogo za ujasiriamali  na wengine wana ufundi  lakini ni wapi wapate vifaa vya kufanyia kazi zao ili waweze kujikimu  kimaisha.
x)                  Kutokuwa na elimu ya kuanzisha miradi na elimu ya kujitegemea maana hata kata zenye umoja na zimekwisha changia pesa na kuwa nazo mfukoni hawazifanyii kitu chochote mfano kikundi cha Runyaga-Chanika wanakiasi cha Sh 60,000  hawana mradi,Bweranyange wanakiasi  cha sh 62,500 hawana  mradi na Ihanda wanakikundi hawana mradi na vikundi vingine vya Kiruruma,Nyakayanja,Nyakasimbi, Kimuli na Kibondo elimu ya kujitegemea inahitajika.
xi)                Kuwepo hali ya kujinyanyapaa wenyewe walemavu kwa kutojitokeza nap engine kuwa na usiri katika kutaja aina ya ulemavu,pia walezi wa watu wenye ulemavu kuwepo na tabia ya kuwafungiana ndani pengine kuona kama ni mkosi kuwa na mlemavu.

xii)              Kuwepo kundi kubwa la wazee waliojitokeza kuwa ni walemavu wakati mwingine ikiwa ni kukabiliwa na hali ngumu kitu kinachotokana na kusauliwa hivyo ndio maana timu hii inashauri kuwepo nguvu ya pamoja tunaamini kuna wadau wanaohusika na kuratibu na kutekeleza sera inayohusu wazee ikitekelezwa vema tutaondoa tatizo hili.

xiii)            Kuwepo na mtazamo hasi kuamini kuwa ulemavu mwingine kuwa ni wa kurogwa jambo ambalo ni hatari kwa jamii kwani hata katika vikundi hawezi kujitokeza.

Ni mengi lakini hayo ni baadhi ambayo tunaona ni makubwa yanayohitaji nguvu ya pamoja ya jamii,wadau wa maendeleo yaani mashirika ya dini,yasiyo ya serikali nay a serikali na serikali yenyewe ili kuweza kuwa na uwiano katika kutoa haki kwa wote kwenye jamii.

Kama ilivyo kawaida ya kazi yoyote ile haiwezi kukosa changamoto za hapa na pale kwani ili ufikie mafanikio lazima ukumbane na vikwazo ukabiliane navyo ndipo uweze kufanikiwa ndiyo  maana bila hivyo hakuna haja ya kuhainga na maendeleo.
Kwanza mtazamo wa jamii kuwa na utegemezi wa kupata misaada,ushirikiana,usiri wa kutoelezea ulemavu walionao,wengine kutaka kujiandikisha tu kwasababu ya kujua kuna chochote.

Wengi wao wanaamini kuwa ulemavu mwingine ni wa kurogwa imani ambayo inachangia sana kutokuwepo takwimu sahihi za watu wenye ulemavu maana hawako tayari kujitokeza kuelezea ulemavu walionao kwa jamii ili waweze kusaidiana katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili.







2        KUWATAMBUA WATU WENYE  ULEMAVU  NA AINA YA ULEMAVU WALIONAO.

Zoezi la kuwatambua watu wenye ulemavu hapa wilayani Karagwe lilianza rasmi tarehe 22.2.2012 katika kata za Rukuraijo, Nkwenda na Rwabwera kwa kuwatembelea katika vijiji vya na kufanyanao mahojiano na kubainisha ni changamoto zipi zinawakabili na nijitihadi zipi wanazifanya katika kukabiliana na changamoto hizo.

Nimengi katika ziara hizi za kuwatambua watu wenye ulemavu tumeyabaini na mengine kuibuliwa ambayo tulikuwa hatuyajui kwani bila kumuuliza mlengwa huwezi juu anakataa nini na anahitaji nini  baadhi tuliyobaini ni,kuwepo idadi kubwa ya watu wenye ulemavu,aina mbalimbali za ulemavu,kutokuwa na umoja unaounganisha watu wenye ulemavu katika ngazi za vijiji hata kata,kutokuwepo ushirikishwaji wa kutosha kwa watu wenye ulemavu kati miradi ya maendeleo na katika maamuzi kwa mambo yanayowahusu kama walengwa wakuu.

Pia tuliweza kufahamu ni mazingira yapi watu wenye ulemavu wanayoishi na hali ya maisha yao kwa ujumla ikiwa inajumuisha   familia zao.Ifuatayo ni jedwali linaloonesha kata idadi ya watu wenye ulemavu ,aina ya ulemavu na kipi kimefanyika katika kusaidia kutatua changamoto na maoni kwa ujumla.


2.1 HALI HALISI YA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA ZIARA YA KUWATAMBUA  HAPA WILAYANI KARAGWE.

Katika ziara ya kuwatambua watu wenye ulemavu tuliweza kubaini mengi kama tulivyokwisha bainisha hapo juu tuliweza kuionea hali halisi na kupata picha kamili juu ya watu wenye ulemavu ni jinsi gani ambavyo ni kundi lenye mahitaji maalumu ambalo linahitaji jitihada za pamoja za mashirika ya umma na ya binafsi,wadau wamaendeleo,serikali na jamii kwa ujumla ili kuleta usawa katika maendeleo kwenye jamii yetu.

 Mengi tumejifunza lakini tuliyoweza kuyabaini ni pamoja na hali ya kipato miongoni mwa familia za watu wenye ulemavu,kipato kuwa duni,kutoshirikishwa kikamilifu katika mambo yanayowahusu,kuwa na utegemezi kutoka kwa ndugu ama kwa familia zao,pia kuwepo na dhana ya imani za kishirikina ambazo kwa kiasi kikubwa zinachangia ulemavu mwingine usingekuwa wa lazima wangeweza kupata matibabu na kupona kabisa na kutojua ni wapi wanaweza kusemea au kuelekeza shida zao zikasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi.

Katika kata hizi hali halisi tuliyoweza kujionea ni kutokuwepo ushiriki wa watu wenye ulemavu katika vikao vya maamuzi na kutokuwa na umoja ambao ungelikuwa ni sehemu ya kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili.
Pia tuliweza kubaini moja kwa moja watu wafuatao wangesaidiwa au kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yao wangeweza kuondokana na matatizo wanayo wakabili.


Wengi wao wanaomba kusaidiwa kupunguziwa michango pengine kutokana na hali duni za maisha walizonazo kutokana na kutokuwa na ukamilifu wa viungo kwani hawawezi kumudu gharama za kuwasomesha watoto pia kuitunza familia kwa ukamilifu.

Umoja wa  watu wenye ulemavu wa kata Bweranyange ungesaidiwa elimu ya mchanganuo mzuri wa kuanzisha mradi ungekuwa ni mkombozi kwa umoja huo kwani wameishaonesha  jitihada zao kwani mpaka sasa wanakiasi cha shilingi 62,500 kutokana na michango kukaa katika mfuko bila kuzifanyia mradi itakuwa na haina faida kwa wanachama hao.

Mfano wa umoja wa watu wenye umoja katika kata ya Bweranyange ungelifaa kuwa moja ya chanzo muhimu cha kuwa na umoja uliodhabiti kwa watu wenye ulemavu hapa wilayani ili kuwa na nguvu ya pamoja.

Wapo baadhi ya walemavu wanaohitaji msaada wa haraka kwa kupata matibabu au kupatiwa msaada kama ule magongo kwani hali zao zinahitaji uangalizi zaidi na wengine wakiwezeshwa wanaweza kujikwamuwa kimaisha kutoka hali duni kwenda hali nzuri.mfano katika kata ya;

1.Bweranyange
i)Pendo  Bita-ambaye ni mtoto ana ugonjwa ambao umesababisha mguu wake
                        kuoza hadi mfupa kutokezea kwa nje hivyo msaada wa matibabu
                         unahitajika haraka

ii)Teleza Joseph-Anahitaji msaada wa matibabu ya miguu maana ina kidonda
                              kinachohitaji matibabu ya haraka na magongo ya kutembelea

iii) Moris  Philibert-Anahitaji msaada wa matibabu.

2.Kibondo
i)Genegeva  Raulian- Ambaye ni mlemavu wa mguu anahitaji msaada wa kuwasom
                                     esha watoto wake 2 mmoja akiwa kidato cha kwana na
                                     kidato cha tatu katika shule ya sekondari Nyabiyonza.


1.NYAISHOZI
i)Beath Christian -ambaye ni mtoto ana ulemavu wa viungo anahitaji msaada wa
                               marekebisho ya wilichair aliyokuwa nayo imeharibika.

ii)Joshua Josephat -Anahitaji msaada wa matibabu ya miguu maana imepooza.                           

iii) Mhubiri  Joseph -Anahitaji msaada wa matibabu ya miguu naye imepooza.
iv)Athanasi  Mtunzi –Ni mlemavu wa macho ana miaka kumi na 18 ana tatizo la
                                        macho anaomba msaada wa matibabu.
2.IHEMBE
  i)Akilina   Respisius –Ana ulemavu wa viungo vyote yeye anaomba akipatiwa
                                      msaada wa wilichair aweze kumudu maisha yake.

ii)Ajuna Joseph- Ana ulemavu wa macho anahitaji msaada wa matibabu ya
                              maana anasoma darasa la nne yanamsumbua.


3.RUGU
   i) Selematus  Tibamanya-Yeye  ni mlemavu wa mguu anaomba msaada wa
                                                kumsomesha  motto wake

 ii)Henericko Bebaiya – Ana ulemavu wa macho yeye anahitaji matibabu.

iii)Steven  Faustine – Yeye ana ulemavu wa kupungukiwa na akili pia ni  bubu
                                     msaada wa kumtunza.
4NYAKASIMBI
i)Abdala   Tomasi-Ana ulemavu wa miguu yeye anahitaji msaada wa baiskeli
                                 kuendesha kwa kunyonga na mikono.
ii)Nzoka  Kagande –Yeye anahitaji msaada wa kusomesha watoto wake,ana
                                    ulemavu wa mkono.

iii)Afrey  Aron –Yeye ni bubu mama wa motto huyu yeye anabainisha kuwa kiu
                            yake ni motto wake ni kupata shule ya walemavu.

iv)Pundensiana Rwanga-Yeye anaomba kujengewa nyumba baada ya kunyanga
                                            nganywa yake alipokuwa Muhimbili kimatibabu.




Na changamoto nyingine ni kutokuwa na umoja ambao ungeweza kusaidia wao kubuni na kunzisha miradi ambayo kwa kiasi Fulani ingeweza kutatua baadhi ya changamoto na pia wangeweza kushirikishwa katika maamuzi.

Moyo wa uzalendo na uadilifu unahitajika katika kuunganisha nguvu za pamoja kutatua hili suala kama Redio FADECO ilivyotoa nafasi kwa watu wenye ulemavu  kupaza sauti zao pia imeweza kuwa mwanzo mpya kwa watu wenye ulemavu kuunda vikundi .


2.2Ifuatayo ni chati inayoonesha takwimu za watu wenye ulemavu na ni mambo yapi wameishafanya katika kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili

KATA

AINA YA ULEMAVU
IDADI
JINSIA
NINI KIMEFANYIKA
MAONI
ME
KE
KIBARE


164
46
66
15 Wanazo fimbo
Waliobakia wana huhitaji wa kusaidiwa fimbo,miwani na wengine mahitaji ya shule haswa 2 mmoja akiwa kidato cha

Miguu 47



za kutembelea


Matende 3






 Akili  15




1 alikuwa na mguu


Mikono 20



wa bandia ila


Macho 11



amezidi umri sasa


Viziwi 8



ni mfupi


Kifua 5






Migongo 4




pili,na


Bega 1




msekondari ya Bugomora


Kichwa 4




Mgonjwa wa


Ngozi  2






Kupooza 7




fistula asaidiwe.


Fistula 1







Nyonga 1







Kifafa 2







Kiwete 1





KANONI

Kichwa
51
36
15




Busha 1



Kuna upendo kwa watu wenye ulemavu.
Uongozi wa kata una hitajika kuongeza nguvu katika kuwaunganisha walemavu.


Mgongo 1







Macho 7







Viziwi







Mikono 7







Kiwete  1







Miguu 21







Akili 5







Ngozi 1







Kupooza 2







Nundu 3





KAMULI

Miguu 32
56
37
19




Mikono 10



Kuna jitihada za kuunda umoja.
Lazima msaada wa kuihamasisha unahitajika.


Akili 3







Viziwi 1
Bubu 2







Kupooza 5





SONGAMBERE

Miguu 14
53
40
13




Mikono 5



Kuna jitihada za kuunda vikundi
Elimu zaidi bado inahitajika kuwasaidia kuwa na umoja imara.


Mgongo 2







Kupooza 12







Ngozi 4







Midomo 2







Bubu 2





NKWENDA


20
14
6




Miguu 10



Elimu ya kuunda umoja na kuanzisha mradi imetolewa
Bado jitihada za wadau na vyombo vya habari zinahitajika


Mikono 5




Chuo cha walemavu cha Muhulirwe kijengewe uwezo kuwasaidia walemavu


Viungo 3







Albino 1







Macho 2











-

RUKURAIJO


20
16
4




Mikono 3



Kuna baadhi ya walemavu wanajishughulisha na biashara ndogondogo.
Tatizo ni mtaji hivyo wawezeshwe upande wa mtaji.


Ngozi(albino)1







Miguu 7







Kichwa 2







Macho 4







Viungo  3





















KIMULI


100
70
30




Mikono 14



Kumeanzishwa umoja ktk kata hii.
Kuna changamoto ikiwa ni pamoja na kutokuwepo usajili wa umoja huo


Bubu 2




Kusaidia katika kuanzisha mradi wa kuingiza kipato.


Miguu 27







Akili 2







Kichwa 6







Viungo  4







Kifafa 3







Macho 12







Kupooza 10







Mgongo 5






Viziwi 5







Masikio 6













NYAKATUNTU


56
30
26




Kifafa 3



Elimu ya utambuzi



Mikono 15




Bado jitihada zinahitajika


Bubu 2







Miguu 13







Akili 4







Macho 7







Kupooza 4







Viziwi  3







Viungo 5





KIKUKURU


31
13
18




Kifafa 2







Mikono 8



Kuunda vikundi elimu imetolewa
Jitihada za serikali na jamii bado zinahitajika


Macho 2







Miguu 10







Akili 2







Kupooza 2







Viungo 5





















IHANDA









Mikono 5
32
20
12




Viungo  5







Miguu 11







Akili 2







Macho 4







Kupooza 2







Kichwa 3













BUSINDE


27                
10
17




Kifafa  1



Kuanzisha vikundi ndilo linafanyiwa kazi
Elimu ya uanzishwaji miradi inahitajika


Mikono 8







Kichwa 2







Miguu 10







Akili 1







Macho 3







Kupooza 2





















BUGOMORA


33
20
13




Mikono 9



Kuna jitihada za baadhi ya watu walioenda hospitalini.
Ushauri bado unahitajika.


Bubu 1







Miguu 12







Operation 1







Akili 2







UgonjwaNgozi 2







Kupooza 6













RUTUNGURU


11
6
5








Kuunda vikundi ndo zoezi linaloendelea.
Elimu ya kujitegemea ni muhimu


Mikono 2







Macho 2







Miguu 5







Akili 1







Viungo 1





















KIBINGO

Miguu 6
13
6
7




Viungo 1



Kuna upungufu kwa uongozi wa kata kutowathamini .
Uongozi unahitaji kuelimishwa juu ya kuwasaidia watu wenye ulemavu.


Macho 2







Mikono 4













MURONGO


16
9
7




Kifafa 2



Kuna upendo wa viongozi kuwatambua watu wenye ulemavu.
Jitihada za waandishi kutembelea kata hii upo maana ipo mpakani na mawsiliano si mazuri.


Macho 4







Miguu 4







Mikono 3







Bubu 3













MABIRA


40
25
15




Mikono 4



Kuna jitihada za kuunda umoja zimeanzishwa
Wadau na serikali ni lazima ziwepo katika kuwaunganisha


Macho 3







Miguu 10







Viungo 3







Akili 2







Kupooza 3







Masikio 4







Kichwa  7







Mgongo 4





RWABWERE


26
14
12




Miguu 6



Kuna jitihada za kuelimisha wanajamii juu ya kutowanyanyapaa
Elimu kwa jamii kuhusu kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu inahitajika


Macho 5







Mikono 6







Akili 2







Kichwa 1







Masikio 4







Kifafa 2





CHONYONYO

Kifafa 2
22
12
10




Macho 3



Hakuna ushirikiano
Uongozi wa serikali una ulazima wa kutoa elimu kwa jamii.


Kupooza 2







Mikono 4







Kichwa 4







Miguu  6







Akili  1
































24
11
13


ISINGIRO

Kifafa 2



Kuna unafuu maana kuna chuo cha ufundi kilichosaidia watu wenye ulema kupata ujuzi
Chuo hiki kingeliendelezwa kwa ajili ya kuwapa fursa watu wenye ulemavu.


Kupooza 2











Macho 4







Viziwi 2







Mikono 4







Bubu 2







Miguu 6







Akili 2





























KAISHO


20
9
11




Akili 2



Jitihada za uongozi wa kata kuwathamini zinaleta hamasa kwao
Kuimarisha umoja wa watu wenye ulemavu  unahitajika


Kifafa 2







Macho 3







Viziwi 1







Mikono 2







Bubu 2







Miguu 8













IGURWA


41
21
20




Kifafa 2



Unafuu wa kusikilizana na kuthaminia upo.
Kuundwe umoja ulio imara kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili.


Macho 10







Viziwi 2







Mikono 6







Viungo 2







Miguu 15







Akili 2







Ngozi 1







Kupooza 1






































KATA
AINA YA ULEMAVU
IDADI
JINSIA
NINI KIMEFANYIKA
MAONI
ME
KE
KITUNTU

43
26
17



Miguu 21






Macho 6



17 Wanafimbo za kutembelea.Japo nyingine ni za kienyeji ambazo hazikidhi matakwa sahihi.

3.Wangepatiwa ufadhili wa baiskeli za watu wenye ulemavu kama walivyoomba.

Matende  1




Mikono 4




Viungo vyote 5




Akili(Taira) 2




Mdomo 1




Ngozi  1




Kiziwi 1




Nundu(ebango)1








CHANIKA

36
22
14



Macho 4



10.Wana fimbo za kutembelea

1.Mmoja alifanyiwa upasuaji wa mdomo wa sungura maendeleo yake ni mazuri

2.Kijiji cha Runyaga wanakikundi chao  cha watu wenye ulemavu
1.Wazazi ambao ni walemavu wangepunguziwa ada kwa watoto wao walioko sekondari
2.Kikundi cha walemavu wangesaidiwa utalaamu wa kuanzisha mradi kama walivyoomba

Mikono 7




Miguu 17




Akili(Taira) 2




Nundu 1




Kifua 1




Mdomo 1




Bubu 1




Kifafa 1




Mgongo 1




Viungo vyote 4















KATA
AINA YA ULEMAVU
IDADI
JINSIA
NINI KIMEFANYIKA
MAONI
ME
KE







KIRURUMA

23
16
7



Macho 2



Baadhi wana magongo ya kutembelea
Wasaidiwe jinsi ya kuanzisha miradi.

Mikono 9



Wameunda umoja wa watu wenye ulemavu.
Wenye mahitaji matibabu ya haraka waelekezwe ni wapi waende.

Kichwa 1



Wanashirikiana kujadili changamoto zinazowakabili.


Ugonjwa wa ngozi 1






Miguu 5






Bandama 2






Mgongo 1






Masikio 1






Viungo  vyote 1












NYABIYONZA

6
4
2



Akili (Taira)1



Kuna mmoja alifanyiwa opereshen
Waidiwe katika kuunda umoja wao.

Miguu 3



Hakuna umaja ktk kata
Washirikishwe ktk maamuzi

Kichwa 2












BWERANYANGE

37
23
14



Miguu 13



Kuna umoja imara wa watu wenye ulemavu.


Macho 8



Kuna mtoto aliyesaidiwa na Redio Fedeco


Mikono 6






Masikio 4






Kifafa 1






Kifua 2






Akili(Taira)1












KIBONDO

37
21
16



Kifafa 1



Umoja upo umeundwa.
Elimu ya kuingiza kipato inahitajika ili waweze kujikimu kimaisha na kujitegemea

Macho 4






Mikono 6






Kifua2






Miguu 19






Akili 3






Kupooza 1






Tumbo 1






Ngozi/alibin 1






Matende 1






Viungo 2






Mdomo wa sungura 1






Kibiyongo 1






Bubu 2






Kichwa1












NYAKABANGA

10
6
4



Mdomo wa sungura 1



Uhusishwaji wa walemavu ni mdogo.
Elimu ya utambuzi ni muhimu kwa watu wenye ulemavu na viongozi wa serikali ya kata

Macho 2




Mgongo 1




Viungo 1






Tumbo 1






Kifua 1






Ngozi(albino)2












NYAKAKIKA

16
9
7



Miguu 11



Bado uongozi wa kata unawanyanyapaa
Lazima elimu juu ya kuondoa vitendo vya unyanyapaa viondolewe.

Kifafa 1






Viungo 1






Mikono 2






Akili(Taira)1










ME
KE









NYAISHOZI

17
8
9



Viungo 2



Mmoja  ana wilichair ila imeharibika inahitaji marekebisho
Wangesaidiwa msaada wa kurekebisha wilichair

Miguu 6




Mikono 2




Macho 3




Kupooza 2




Kifafa 1




Kichwa 1



Kuna watoto wawili wamepata matibabu ila bado kunahitajika msaada zaidi.
Watoto wapatiwe msaada wa matibabu zaidi ili waweze kuendelea na shule.















































IHEMBE

22
15
7



Bubu 2



Tumewapatia elimu ya kujiunga katika vikundi
Wangesaidiwa wenye mahitaji ya matibabu.

Viungo 4




Miguu 6




Mikono 4



Wabuni na kuanzisha miradi


Macho 2




Tumbo 2




Akili  1












RUGU

43
31
12



Kichwa 4



Kuna baadhi wamepata matibabu ila bado hali si nzuri.
Elimu ya kuanzisha vikundi tumeitoa
Kuna baadhi ya watu wenye ulemavu wanahitaji msaada wa matibabu zaidi.

Ngozi 4




Miguu 12




Kiziwi 1




Kifua 2




Masikio 1




Akili 2



Macho 3




Mikono 6




Viungo 5






Kifafa  2






 Magoti 1



















NYAKASIMBI

29
19
10



Kifafa 1



Wameisha unda umoja wa watu wenye ulemavu ngazi ya kata.
Wasaidiwe namna ya kuwa na kuwa na vyanzo vya mapato.

Mikono 5




Macho 3




Mgongo 1




Viungo 5




Kupooza 2




Akili 1



Wapo  ambao wameisha enda hospitali kwa jitihada zao.
Wasaidiwe elimu ya kujitegemea ili waweze kuondokana na mtazamo wa misaada na utegemezi.

Bubu 1




Nyonga 1




Masikio 1




Miguu 9








RUGERA

42
28
14



Mikono 7        






Miguu 13






Bubu 3



Kuna jitihada za kuunda umoja.
Elimu ya kujitegemea ya kubuni na kuanzisha miradi mbalimbali inahitajika.


Macho5




Kupooza 6




Mgongo 3








NYAKAHANGA

14
8
6



Bubu 1



Elimu ya kuanzisha vikundi imetolewa
Elimu ya ushiriki katika shughuli za maendeleo kwa watu wenye ulemavu.

Viungo 3




Mikono 4




Nundu 1




Miguu 5





KIHANGA

12
9
3



Bubu  2



Jtihda za kuunda umoja zipo
Elimu zaidi inahitajika.

Viungo 1






Macho 2






Miguu 4






Mikono 1






Masikio 1






Kichwa 1












KAYANGA

12
8
4



Miguu 4



Jitihada bado ziko nyuma sana inabidi bidii iongezwe maana ndio makao makuu hivyo kuwe ndio mfano.
Uhamasishaji unahitaji ili watu waweze kutambua wajibu wao katika kusaidia kutatua matatizo ya watu wenye ulemavu.

Kupooza 2




Mikono 3




Viungo 2




Akili 1




















NDAMA

84
57
27



Viwete2



Hakuna jitihada za madhubuti za kuunda umoja
Jitihada za kuunda umoja katika kata hii zinahitaji kwa wahisani wote kushirikiana na watu wenye ulemavu.

Mikono 21




Akili 4




Kupooza 2




Miguu28




Bubu 3




Macho14




Masikio 5




Kifua 1




Shingo 2










BUGENE

100
78
22



Macho 18



Elimu imetolewa ya utambuzi
Jitihada za wanahabari na wadau  ni muhimu kutatua changamoto za watu wenye ulemavu

Akili  5




Jamii pia inahitajika kuelimishwa juu ya wajibu wao

Kupooza 7





Bubu 2





Viungo 6





Miguu 45




Mikono 12











KYERWA

50
26
24



Kifafa 5



Elimu ya kuunda vikundi ilitolewa
Elimu ya kubuni na kuanzisha miradi inahitajika.

Miguu 15






Mikono 16






Kichwa 4






Viungo 5






Bubu  1






Macho 4








2.3 WADAU TULIOWABAINI KATIKA WILAYA YA KARANGWE NA NJE YA KARAGWE KWA AJILI YA KUSHIRIKIANA KUTATUA MATATIZO YA WATU WENYE ULEMAVU.

Katika zoezi hili tuliweza kubaini wadau ambao wanaweza kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kutatua matatizo ya watu wenye ulemavu  ili kuleta umoja na mshikamano wa kukuza sauti zaidi kwani tulichokibaini kuna wadau wngine wanashughulika na msuala ya watu wenye ulemavu moja kwa moja.

Wadau hao ambao tukiunganisha nguvu kwa pamoja tunaweza kuinua sauti zao na kuimarisha hali zao hao ni KCBR, SAWAKA, HALMASHAURI  YA WILAYA,VYOMBO VYA HABARI,AFYA na Jamii kwa ujumla.
KCBR ni shirika linalohusika na shughuli za kuwahudumia watu wenye ulemavu wilayani hivyo tukiweza kushirikiana kwa pamoja uwezekano mkubwa wa kupaza sauti kwa pamoja ili kutetea haki za watu wenye ulemavu pia kuinua hali za maisha yao.
SAWAKA tulichokibaini katika zoezi hili ni kuwa kuna wazee ambao wanaulemavu ambao shirika hili la sawaka ambalo linajihusisha na masuala mazima ya kuwa  hudumia wazee wanaweza kusaidia katika kupunguza matatizo katika upande wa watu wenye ulemavu kwa ajili ya kusaidiana kutatua matatizo yanayokabili watu hao.
HALMASHAURI ZA WILAYA tumeweza kubaini kuwa tukishirikiana vizuri na halmashauri zote hapa nchini kupitia vitengo vya maendeleo ya jamii,ustawi wa jamii kwani tumebaini hivyo ni kuwa maendeleo ya jamii maana wanaguswa moja kwa moja kutambua makundi yenye mahitaji maalumu,na upande wa ustawi wa jamii ni kwa ajili ya sera ya matibabu kwa watu wenye ulemavu zenasemaje hivyo tunaweza kushirikiana kuwasaidia watu wenye ulemavumaana wengi wao wanashindwa kupata matibabu kwasababu hawajui wafanye nini.

VYOMBO VYA HABARI tumebaini kuwa vyombo vya habari vikitimiza lengo lake kwa ukamilifu kazi zake ambazo ni uelimishaji,kuhabarisha na kuburudisha tunaweza kuisaidia jamii kwa ujumla. Najua waandishi wa habari na vyombo vya habari wakikaa kwa pamoja tunaweza kuihdumia  jamii kwa ufasahau zaidi.

2.4  MAPENDEKEZO NA MAONI YA JUMLA KWA ZOEZI HILI LA UTAFITI NA ZIARA ZIMA  NINI KIFANYIKE.

i)Kwanza elimu ya kuanzisha umoja ngazi za kata itolewe kwa watu wenye ulemavu wao wenyewe ili waunde umoja wao utakaowasaidia katika kutatua baadhi ya changamoto kama vile kutoshirikishwa katika shughuli za maendeleo.

ii)Elimu ya kubuni na kuanzisha miradi itolewe pia ili kuwepo na hamasa ya kujiunga kwenye umoja waweze kuunganisha nguvu katika kutatua matatizo yao na kujikimu kimaisha kuliko kutegemea misaada ambayo huwa ni ya muda hivyo wajengewe uwezo wa kujitegemea

iii)Vyombo vya habari na waandishi wa habari wapatiwe mafunzo maalumu ya jinsi gain ya kuripoti vema na kuandaa vipi vyenye kugusa moja kwa moja maisha ya watu wenye ulemavu kwa ufasaha na kuepuka lugha ambazo zinaweza kuleta unyanyapaaji na utengano miongoni mwa watu wenye ulemavu.

iv)Mashirika ya kidini,yasiyo ya kiserikali,wadau wa maendeleo,jamii na serikali kwa ujumla washiriki kwa pamoja kuunganisha nguvu kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu.

v)Wasaidiwe katika kutetea na kutekelezwa kwa sera mbalimbali zinazohusu watu wenye ulemavu katika kupata huduma za matibabu,kukopeshwa ikiwezekana kupitia vikundi vyao waungane kuanzisha SACCOS YAWALEMAVU WILAYA.

vi)Kwa kata ya Bweranyange wameonesha mfano wakuigwa  maana uongozi wa kata hiyo unawashirikisha watu wenye ulemavu kwa maana katibu wa umoja wa watu wenye ulemavu ndiye pia katibu wa baraza la kata.Pia diwani wa kata hiyo na afisa kata kuwapa kipaombele ni mfano wa kuigwa na viongozi wengine ili uwe kama majaribio ya kata nyingine kwenda kujifunza na si karagwe tu bali Tanzania.

vii)Umoja wa watu wenye ulemavu wa kata ya Nyakasimbi  ujengewe uwezo na kuendelezwa zaidi ili uwe na manufaa na chombo cha kusaidia watu wenye ulemavu katika kata yao pia unaweza kuchukuliwa kama eneo la mfano wa kuanzisha umoja kama huo kwa kata za Ihembe,Rugu na Nyaishozi kwa lengo la uongozi wa kata uwatambue na kuwashirikisha katika maamuzi ya maendeleo na mambo yanayowahusu moja kwa moja ,pia kutetea na kutekeleza sera mbalimbali zinazogusa mambo yao.

viii)Kwa umoja wa kata za  Nyakasimbi,Kiruruma,Kimuli,Kibondo,Ihanda, na baadhi ya matawi ya kata za Chanika mfano Runyaga na Kata ya Nyaishozi katika kijiji cha Nyakayanja zijengewe uwezo na kuimarika ili kuwepo na umoja ulio imara katika kutatua changamoto zinazowakabili.

ix)Watoto wenye ulemavu ambao wanahitaji shule zenye kuhudumia watoto wenye ulemavu wasaidiwe kutafutiwa nafasi katika shule hizo  walioko katika kata za
Chanika, Nyakasimbi,Rukuraijo,Rutunguru ambao wameishajaribu kwenda Mgeza hawajafanikiwa kupata nafasi.

x)Wanaohitaji msaada wa haraka kimatibabu pia wapatiwe ufumbuzi wa haraka ili kuwasaidia kurudi katika hali zao za awali.Mfano watoto wawili wa Bugomora wenye ugonjwa wa ngozi ,na Pendo Bita wa Bweranyange mguu ambao unaoza unaweza kutibiwa.

xi)Chuo cha ufundi kilichopo eneo la Muhulirwe katika kata ya Nkwenda kilicho chini ya uongozi wa walemavu kiboreshewe miundo mbinu kwa upande wa vifaa maana wanacherehani za kukodi hivyo wapatiwe zao ili kiweze kuwahudumia watu wenye ulemavu kikamilifu.

2.5  HITIMISHO.

Tunahitimisha kwa kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia kujionea hali halisi ya maisha ya watu wenye ulemavu kwa kiasi kikubwa inahitaji moyo wa uadilifu mkubwa katika kuwahudumia ,kuwafariji na kuwapa msaada wa ushauri.

Pia tunapongeza jitihada za mkurugenzi wa REDIO FADECO bwana Joseph Sekiku za haraka za kuwasaidia watu wenye matatizo ya FISTULA NA MDOMO WA SUNGURA kwani mama mmoja toka Kigorogoro tiyari yuko jijini Dar es salaam akitibiwa na shirika la CCBLT ni mara tu baada ya kuwatambua na kwenda huko kuona ni jinsi gain wanaweza kuwasaidia.

Tunashukuru sana kwa viongozi wale wote waliokuwa mstari wa mbele kutupokea kwa upendo na kuonesha kuwajali watu wenye ulemavu mfano wao akiwa ni uongozi nzima wa kata ya Bweranyange chini ya diwani wake Yusufu Kagande,Saby Rwazo wa kata ya Kanoni,Uongozi wa kata ya Kiruruma ,kata Kaisho,Kimuli, Rurukuraijo,Murongo,Kibare na Kata nyingine ambazo kwa kiasi kikubwa zilijitahidi katikakuwajali watu wenye ulemavu
. Jamii na uongozi wa kuanzia kitongoji mpaka Taifa kwa ujumla inatakiwa kulifanya suala la watu wenye ulemavu kuwa mtambuka kwa kila kikao lijadiliwe na pia kuwahusisha katika vikao vya maamuzi kwa mambo yanayowahusu na maendeleo kwa ujumla.Na sera zinazohusu watu wenye ulemavu ziangaliwe na zitekelezwe kwa kikamilifu ili kutatua matatizo yanayowakumba watu wenye ulemavu.
Tunaomba nguvu kutoka kwa wadau wote kulifanya zoezi hili liwe ni suala mtambuka hivyo liwe ni moja ya agenda kuu katika vikao vyote pia kuunganisha nguvu kwa ajili ya kulifanya liwe endelevu hata ikiwezekana iwe mkoa wa Kagera wote na Tanzania kwa ujumla.

IMEANDALIWA NA JUHUDI  FELIX
   

No comments:

Post a Comment