Friday, April 20, 2012

KUMBE VIJANA TUKIJIBIIDISHA INAWEZEKANA KUUAGA UMASKINI

Vijana katika kata ya kiruruma wamesema kuwa kupitia  mradi wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) wameweza kujipatia ajira na kuinua vipato vyao kutokana na ufugaji wa kuku.

Wakizungumza jana na waandishi wa habari katika kijiji cha Kamagambo walisema kuwa mradi wa ufugaji wa Kuku uliibuliwa katika mkutano mkuu wa serikali  ya kijiji  kwa kushirikiana na Tasaf kwa lengo la kusaidia  vijana wasio na ajira.

Walisema kuwa kupitia mradi wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) vijana wameweza kujipatia ajira na kuinua vipato vyao kutokana na ufugaji wa Kuku, ambapo walieleza kuwa kikundi chao kina jumla ya vijana 15,  Wakiume 7. na wakike 8. Kwa mjibu wa vijana hao walisema kuwa walipewa Kuku 6. kila mmoja na kuwa wameweza kuwazalisha na kuwatunza  vizuri ambapo kwa sasa wana jumla ya kuku 264  na kuwa tangu mradi uanze wameisha uza Kuku zaidi ya 120.

Mmoja wa wanakikundi Bi, Madina Hussein ambaye pia ni mhazina wa kikundi alisema kuwa wamekuwa wakishirkiana  kwa pamoja ili kuufanya mradi wao kuwa endelevu na kuiletea jamii tija na faida kubwa.
Bi; Hussein aliongeza kuwa kabla ya mradi huo vijana walikuwa wakitumia muda wao mwingi katika kucheza mpira karata, na ulezi wa mara kwa mara kuwa kwa sasa  vijana wanajishughulisha kwa ajili ya maendeleo yao.

Alizitaja baadhi ya faida ambazo wamezipata kutokana na ufugaji wa Kuku kuwa ni pamoja na mbolea, ujenzi wa nyumba ya kisasa, matumizi  yangu mbona lishe bora kutoka katika mayai, na nyuma kama kitoweo.

Kwa upande wake, mmoja wa wafugaji hao Bwana Nassoro Beyeza alisema kuwa wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na jamii husika kutokubaliana na mradi  huo kuwa unawaharibia mazao magonjwa yanayo shambulia kuku na kupunguza idadi ya kuku walio  kuwa nao, uhaba wa chakula cha kuku na maeneo ya kuwafugia.

Aidha amewashauri vijana katani humo kujiunga katika vikundi vya maendeleo na uzalishaji kama ilivyo katika miradi ya TASAF ili iweze  kuondokana na utegemezi pamoja na umasikini.

Hata  hivyo, ameitaka TASAF kuwaongezea idadi ya  Kuku katika mradi wao li vijana wenzao waweze kujiunga katika miradi inayotolewa, ambapo amewataja  vijana wote kuwa wavumilivu katika miradi kwa kuijali ili iwawezeshe kuwaongezea uzalishaji.

No comments:

Post a Comment