Friday, April 20, 2012

TASAF KARAGWE YAWAJALI WAZEE

Jumla ya wazee 14 kutoka Kata ya Rwabwere Wilayani Karagwe wamesema kuwa mradi wa ufugaji wa Ng’ombe wa maziwa umeweza kubadili maisha yao kiuchumi na kiafya.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa mradi huo Bw. Sostenes Rweyongeza Valentin kutoka kikundi cha Tuvumiliane kilichopo katika Kata ya Rwabwere wakati alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Katani humo.

Bw. Valentin alisema kuwa jumla ya wazee 14 kutoka Kata ya Rwabwere wameweza kunufaika na mradi wa ufugaji wa Ng’ombe wa maziwa kwa kubadili maisha yao kiuchumi na kiafya ambapo alieleza kuwa wazee hao wameweza kunywa maziwa yanayotokana na Ng’ombe hao na kuwa na afya njema ni pamoja na kujipatia fedha kutokana na maziwa.

Mwenyekiti wa mradi huo Bw. Valentin alisema kuwa mradi wa ufugaji wa Ng’ombe wa maziwa uliibuliwa na mkutano wa Serikali ya Kijiji mwaka 2009 kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Alisema kuwa mradi huo uliwapa Ng’ombe 4 mitamba 3 na dume 1 kuwa kwa sasa wanao jumla ya Ng’ombe 8 ambao wamewatumia kuboresha mashamba yao kwa kutumia samadi inayotokana na wanyama hao.

Pia alisema kuwa wazee hao awali walikuwa hawajiwezi kiuchumi, lakini kwa sasa wanaweza kupata mahitaji yao ya lazima katika familia zao kutokana na mauzo ya maziwa.

Mmoja wa wana kikundi hao Bw. Revelian Rwezaula alisema kuwa mradi huo wa ufugaji wa Ng’ombe umeweza kuwaongezea heshima wazee hao kutokana na mazizi ya mifugo hao inayokuwa katika makazi yao.

Bw. Rwezaula alieleza kuwa shughuli wanazozifanya mara kwa mara katika kuwahudumua mifugo yao zimeweza kuwapa mazoezi ya kutosha na kuimarisha afya zao, ambapo pia ameipongeza TASAF kwa kuwajengea mazizi bora na yaliyo imara.

Aidha, wazee hao wamezitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni kutopatikana kiurahisi madawa ya kuogeshea mifugo yao na waliongezea kuwa baadhi ya wazee hawana mazizi yaliyo bora na imara kama yaliyokuwa yamejengwa na TASAF jambo linalopelekea wazee hao kupata usumbufu katika kudhibiti mifugo yao.

Hata hivyo, wameitaka TASAF kuwaongezea idadi ya ng;ombe kuwa idadi ya wazee katika Kata hiyo ni kuwa ukilinganisha na idadi ya Ng’ombe walio kwenye mradi huo, Kata ya Rwabwere inasadikiwa kuwa na wazee 90 wenye umri kuanzia miaka 60.

1 comment:

  1. Ahsante sana Juhud Felex kwa hayo yote ulioeleza kwani wazee ni rasilimali zetu ambao husaidi katika jamii yeyote.

    Waziri mkuu mizengo Pitter Pinda wamewahi kusema kuwa uthamini wa wazee huonekana baada ya familia kugombana swali Kwanini Uthamani usionekane hata wakati wa raha na kuwajali??????????

    Tafsir ya wazee iwe njia ya kutatua matatizo yao kwani nawe ndio njia utakayo pitia hatakama sasa unajiona unanguvu kibao.

    Waungana wasomaji wa mitandao kila mtu atakuwa mzee hii haihitaji ufafanuzu lakini unategenmea utasaidiwa nanani wakati wewe kwasasa hausaidii waliozeeka?????????????

    Hata biblia inasema kila mtu atalitwa kulingana na kazi yeke Ole wao wayasikiao haya bila kuya jali nao hawatajali wa wakati wa uzee wao

    ReplyDelete