Jumla
ya waendesha vyombo vya moto 901 katika
tarafa za Bugene na Nyaishozi wilayani Karagwe mkoani Kagera wamehitimu mafunzo ya usalama barabarani
yalikuwa yanaendeshwa na taasisi ya
Future World Vocational Insitute kutoka Dar Es Salaam kwa kushirikiana na Jeshi
polisi wilaya ya Karagwe.
Mafunzo
hayo yaliyoanza tangu disemba 05 mwaka huu katika kata za Nyaishozi, Kayanga
na Bugene yamehitimishwa jana huku wahitimu wa mafunzo hayo wakikabidhiwa
vyeti na kutwakiwa kuzingatia waliyofundishwa ili kupunguza au kukomesha kabisa
ajali za barabarani.
Akiongea
wakati wa kufunga mafunzo hayo mkuu wa polisi wilaya ya Karagwe Mika Makanja
alisema mafunzo hayo waliyopata
waendesha vyombo vya moto yatakiwa msaada kwao kama watayatumia inavyotakiwa na
si vinginevyo.
Mkuu
wa wilaya ya Karagwe Deodatus Kinawiro ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji
wa mafunzo hayo alieleza jitihada za
serikali katika kushirikiana wadau wengine kuleta mafunzo kama haya ambayo
anaamini kuwa yatakuwa msaada kwa waendesha vyombo vya moto na watumiaji
wengine wa barabara.





No comments:
Post a Comment